K OCHA Mkuu wa Kagera Sugar ya mkoani Kagera, Francis Baraza amesema kuwa Simba wana nafasi kubwa ya kupindua matokeo kwenye mch...
KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar ya mkoani Kagera, Francis Baraza amesema kuwa Simba wana nafasi kubwa ya kupindua matokeo kwenye mchezo wa marudiano hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kupigwa leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa.
Simba ina kazi kubwa ya kupindua matokeo kwenye mchezo huo ambapo ilikubali kipigo cha mabao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Afrika Kusini kikiwa ni kipigo kikubwa kwa timu hiyo msimu huu kwenye mashindano yote.
“Kwenye mpira chochote kinawezekana, Simba wanayo nafasi kubwa ya kupindua matokeo dhidi ya Kaizer kutokana na rekodi yao wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani pia aina ya wachezaji walio nao kikosini.
“Wachezaji kama Chama(Clatous), Luis (Miquissone), Morrison (Bernard) na Mugalu, (Chris) ni baadhi ya wachezaji ambao wanaweza kukupa matokeo muda wowote kutokana na uwezo wao mkubwa walionao, kikubwa waingie kwa tahadhari kubwa kuhakikisha hawaruhusu bao la mapema kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa kwanza,” alisema Baraza.
Simba wataingia kwenye mchezo huo wakiisaka rekodi yao ya mwaka 1979 ambapo walifanikiwa kupindua meza ugenini baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mufulira Wanderers ya Zambia.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS