UONGOZI wa Simba umesema kuwa ikiwa wachezaji hawatajitoa katika mchezo wao ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs utakaoc...
UONGOZI wa Simba umesema kuwa ikiwa wachezaji hawatajitoa katika mchezo wao ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs utakaochezwa Uwanja wa Mkapa itakuwa ngumu kwao kushinda.
Simba ina kibarua cha kusaka ushindi wa mabao zaidi ya matano katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa Mei 22.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa FNB Soccer City, Simba ilishuhudia ubao ukisoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wanaweza kufanya kila kitu na kuahidi fedha ndefu ila wachezaji wasipoamua hawatashinda.
"Ikiwa tutafanya kila kitu kwa ajili ya mchezo wetu na tukawekeza kwa asilimia kubwa kama wachezaji hawataamua kujituma na kufanya kweli basi itakuwa ngumu kwetu kushinda.
"Wachezaji wana jukumu la kujitoa zaidi ya asilimia 100 na zaidi katika kusaka ushindi na tunaamini kwamba inawezekana. Mchezo wetu wa mwanzo ugenini tulimiki mpira sawa nakubali lakini hatujashinda," amesema Manara.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS