Rais Samia: Makosa Yasitumike Kama Kitega Uchumi
HomeHabari

Rais Samia: Makosa Yasitumike Kama Kitega Uchumi

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amelitaka jeshi la polisi kujielekeza zaidi kutoa elimu badala ya kutumia sh...

Nafasi Mpya za Kazi Serikalini,NGOs na Makampuni Binafsi
Mwalimu wa mazoezi akamatwa kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake
Waziri Mkuu Majaliwa Akutana Na Mwenyekiti Wa ACT Wazalendo Juma Duni Haji

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amelitaka jeshi la polisi kujielekeza zaidi kutoa elimu badala ya kutumia sheria zao kutoza faini. .

Rais Samia amesema hayo leo Mei 18, 2021 wakati akizindua kiwanda cha ushonaji cha jeshi la polisi kilichopo kilichopo katika Bohari Kuu ya Jeshi la Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam.

“Takwimu zinasema kuna upungufu wa makosa na upungufu wa makusanyo ya pesa kutokana na upungufu wa makosa, nataka nielekeze kwamba kazi ya Jeshi la Polisi ni kudhibiti makosa, tusijielekeze sana kwenye kipengele cha makosa na adhabu kwamba ni kitega uchumi, zaidi zitumike kudhibiti kuliko ukusanyaji wa faini na tozo nyingine. Nihimize suala la elimu kwa raia, naona vipindi vyenu kwenye TV lakini naomba muongeze zaidi.

Kuhusu hali ya usalama nchini, Rais Samia Suluhu Hassan amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro kwa kutekeleza agizo lake alilolitoa hivi karibuni la kutaka kudhibitiwa kwa vitendo vya uhalifu ambavyo vimekuwa vikijitokeza katika maeneo mbalimbali nchini.


Hata hivyo, ametaka kudhibitiwa kwa  wale wote wanaolijaribu Jeshi la Polisi kwa kuendeleza vitendo vya uhalifu.

“Baada ya kutoa ile kauli yangu kuhusu wahalifu IGP ulifanya mkutano na kuweka mikakati, lakini tunasikia bado kuna wanaojaribu kina cha maji, wanabonyeza bonyeza, nawaomba mjipange, wakibonyeza pasibonyezeke, kama mliweza huko nyuma hamuwezi kushindwa sasa. " Amesema

Rais Samia  ameongeza kuwa kuanzia sasa miongoni mwa vigezo atakavyotumia katika kuwapandisha vyeo Makamanda wa polisi  ni namna ambavyo wamekuwa wakikabiliana na vitendo vya uhalifu katika maeneo yao.

“Hii sio kwa Dar es Salaam tu, bali nchi nzima, miongoni mwa vigezo tutakavyovitumia kuteua au kutengua Makamanda wa Polisi wa Mikoa ni kasi ya kudhibiti vitendo vya uhalifu, kwahiyo mkajitahidi kudhibiti vitendo vya ujambazi,” amesema Rais Samia.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Rais Samia: Makosa Yasitumike Kama Kitega Uchumi
Rais Samia: Makosa Yasitumike Kama Kitega Uchumi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjp5yuW5gxhRbHvATb0ItYHzwvTzzcXvkA_JP7gHwmbMpSzmL7OLfDv3Ypcl3Cdnzek5EutGtkgX4Mqj4GeM05AvydOOidQdOFZE8Wgd8XfxKB-Llf1OXMUUuazkk2Aj0bM_gPqlfFe9Kp0/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjp5yuW5gxhRbHvATb0ItYHzwvTzzcXvkA_JP7gHwmbMpSzmL7OLfDv3Ypcl3Cdnzek5EutGtkgX4Mqj4GeM05AvydOOidQdOFZE8Wgd8XfxKB-Llf1OXMUUuazkk2Aj0bM_gPqlfFe9Kp0/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/05/rais-samia-makosa-yasitumike-kama.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/05/rais-samia-makosa-yasitumike-kama.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy