GUARDIOLA HAITAKUWA KAZI NYEPESI MBELE YA PSG
HomeMichezo

GUARDIOLA HAITAKUWA KAZI NYEPESI MBELE YA PSG

PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amesema kuwa mchezo wake wa leo Jumanne dhidi ya PSG hautakuwa mwepesi licha ya ule wa awali ...


PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amesema kuwa mchezo wake wa leo Jumanne dhidi ya PSG hautakuwa mwepesi licha ya ule wa awali kuweza kushinda kwa mabao 2-1.

Mchezo wa leo ni wa Champions League ikiwa ni nusu fainali ya pili na mshindi wa jumla atatinga fainali ambapo PSG inakumbuka kwamba ilipoteza mchezo wa nusu fainali ya kwanza ilipokuwa nyumbani. 

Imekuwa inaonesha kwamba City ina nafasi ya kutinga hatua ya fainali kutokana na ubora wa wachezaji wake pamoja na mbinu za Guardiola akiwa ndani ya Uwanja wa Etihad jambo ambalo ameliweka wazi kwamba sio jepesi.

Vinara hao wa Ligi Kuu England wanapewa pia nafasi ya kutwaa taji hilo ambalo lipo mikononi mwa Liverpool inayonolewa na Kocha Mkuu, Jurgen Klopp ambaye hana mwendo mzuri kwa sasa katika kutetea taji hilo kutokana na kuandamwa na wachezaji wake wengi ambao wanasumbuliwa na majeraha.

Kocha Mkuu wa PSG, Mauricio Pochettino amesema kuwa utakuwa ni mchezo mgumu kwa pande zote mbili bila kujali nani yupo nyumbani kutokana na ubora wa wachezaji waliopo.

"Hautakuwa mchezo mwepesi kwa timu zote mbili hasa ukizingatia kwamba kila upande una wachezaji wazuri, tupo tayari kwa ajili ya ushindani na tutapambana kufanya vizuri,".

 Guardiola amesema kuwa itakuwa ngumu kwake kuweza kulinda kiwango cha wachezaji wake mbele ya PSG inayonolewa na Mauriccio Pochetino.

"Haiwezekani kuweza kuendelea kuwa kwenye kiwango bora kama awali na huwezi kutabiri kuhusu mchezo wetu mbele ya PSG nina amini kwamba utakuwa mchezo mgumu na jambo lolote linaweza kutokea ndani ya dakika 90.

"Sio tofauti na wakati ule ambao tumefanya vizuri ila kuna kitu cha kipekee ambacho kitafanyika, kiuhalisia ni ngumu  timu ambazo zinashiriki Ligi Kuu England ubora wake ni sawa na  ule wa PSG hivyo huwezi kutabiri,".
Mchezo wa leo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 10:00 usiku.





Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: GUARDIOLA HAITAKUWA KAZI NYEPESI MBELE YA PSG
GUARDIOLA HAITAKUWA KAZI NYEPESI MBELE YA PSG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhcDFddz1I26sPTjRWnk9JKJlmny_EVFZ50BdidbF8y-Xbl4cKk1Hj2LhSq7AIslUubdcMUyxfyf04VeuwBTx2juWf85MhLoluIVUY_Xdki-iLTIdilKTKOSJayCb-6CHSRQrtab072ftwY/w640-h466/City+tena.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhcDFddz1I26sPTjRWnk9JKJlmny_EVFZ50BdidbF8y-Xbl4cKk1Hj2LhSq7AIslUubdcMUyxfyf04VeuwBTx2juWf85MhLoluIVUY_Xdki-iLTIdilKTKOSJayCb-6CHSRQrtab072ftwY/s72-w640-c-h466/City+tena.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/05/guardiola-haitakuwa-kazi-nyepesi-mbele.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/05/guardiola-haitakuwa-kazi-nyepesi-mbele.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy