BAADA ya kumaliza kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Kagera Sugar kikosi cha Simba kimetua Mwanza kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu ...
BAADA ya kumaliza kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Kagera Sugar kikosi cha Simba kimetua Mwanza kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Gwambina FC.
Ubao wa Uwanja wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 0-2 Simba ambapo watupiaji walikuwa ni Luis Miquissone na Chris Mugalu.
Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa kesho, Aprili 24, Uwanja wa Gwambina Complex.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Simba 3-0 Gwambina FC na kufanya wapinzani hao kuacha pointi tatu kwa Mkapa.
Kwenye msimamo wa ligi, Simba ipo nafasi ya pili na ina pointi 55 baada ya kucheza mechi 23 huku Gwambina FC ikiwa nafasi ya 12 na ina pointi 30 baada ya kucheza mechi 25.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS