MINO Raiola, wakala wa mchezaji wa Klabu ya Borussia Dortumund, Erling Haalad amesema kuwa timu hiyo haitamuuza mchezaji huyo. Raiola a...
MINO Raiola, wakala wa mchezaji wa Klabu ya Borussia Dortumund, Erling Haalad amesema kuwa timu hiyo haitamuuza mchezaji huyo.
Raiola amesema kuwa anafahamu mabosi wa mchezaji huyo hawana mpango wa kumuuza Haalad ambaye amekuwa akitajwa kuwekwa kwenye rada za timu kubwa zinazoshiriki Ligi Kuu England.
Miongoni mwa timu ambazo zinatajwa ni pamoja na Manchester United, Chelsea. Liverpool na Manchester City.
Wakala huyo amesema kuwa haliwezi kuwa suala jepesi kwa staa huyo kuondoka kwenye timu anayoitumikia kwa sasa.
"Naheshimu maamuzi yao lakini ipo wazi kwamba klabu yake haitaki kumuuza mshambuliaji huyo kwa sasa," .
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS