DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anatambua mchezo wa leo dhidi ya JKT Tanzania utakuwa na ushindani mkubwa ila amewaambia w...
DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anatambua mchezo wa leo dhidi ya JKT Tanzania utakuwa na ushindani mkubwa ila amewaambia wachezaji wake wanapaswa kupambana ili kupata pointi tatu.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, ubao ulisoma JKT Tanzania 0-4 Simba baada ya dakika 90.
Huku bao la kwanza la Luis Miquissone akiwa nje ya 18 likiwa ni moja ya bao bora na kushangilia kwa kuwafuata mashabiki kulimponza nyota huyo ambapo alionyeshwa kadi ya njano.
Gomes amesema:"Utakuwa mchezo mgumu ila tunahitaji pointi tatu muhimu,ushindi wetu ni mwanzo wa kuendelea kupunguza pointi ambazo tunadaiwa na wapinzani wetu.
"Ukweli ni kwamba kila timu ambayo tunakutana nayo ndani ya uwanja inafanya vizuri katika kusaka matokeo hivyo nasi kazi yetu ni kusaka ushindi,".
JKT Tanzania kwenye msimamo ipo nafasi ya 10 ina pointi 24 baada ya kucheza mechi 21 inakutana na Simba iliyo nafasi ya pili na pointi zake ni 42.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS