MANCHESTER UNITED YATAJA UCHOVU KUWA SABABU YA KUCHAPWA MABAO 3-1 FA
HomeMichezo

MANCHESTER UNITED YATAJA UCHOVU KUWA SABABU YA KUCHAPWA MABAO 3-1 FA

KOCHA Mkuu wa Manchester United,  Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa hawakuwa na namna ya kuweza kushinda mchezo wao wa Kombe la FA mbele y...


KOCHA Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa hawakuwa na namna ya kuweza kushinda mchezo wao wa Kombe la FA mbele ya Leicester City kwa kuwa wachezaji wake walikuwa wamechoka.

Solksajer amesema kuwa wachezaji hawakuwa na maajabu kwenye mchezo huo kwa kuwa ni muda mfupi wametoka kucheza na wamesafiri muda mrefu jambo ambalo limewafanya washindwe kuonyesha makeke yao uwanjani.

United imetolewa kwenye Kombe la FA hatua ya robo fainali kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Leicester City ikiwa ni siku tatu baada ya kutoka kushinda kwenye mchezo wa Europa League mbele ya AC Milan pale San Siro na United ilishinda bao 1-0 ambalo lilifungwa na Paul Pogba.

Mabao ya Leicester City yalifungwa na Kelechi Iheanacho dakika ya 24 na 78 na Youri Tielemans dakika ya 52 huku lile la Manchester United likifungwa na Mason Greenwood dakika ya 38.

Kocha huyo amesema kuwa hali inaeleweka kwa wachezaji namna walivyo pamoja na kushindwa kushinda Uwanja wa King Power kwa kuwa wanacheza mechi moja kila baada ya siku tatu jambo lisilo la kawaida.

"Hatukuwa na chaguo na inaeleweka kwamba kila baada ya siku tatu wachezaji wanacheza na hilo ni jambo kubwa na kila mechi ina ushindani. Tumekuwa tukitumia muda pia kwenye safari kwa kuwa tunahitaji kufanikiwa ni lazima hili tulimudu kwenye maisha yetu ya soka.

"Ni lazima tujifunze na tuwe na hali ya kujiamini kwa ajili ya mechi zetu zijazo, kazi bado ni ngumu na mechi zinatukabili kila wakati," .



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: MANCHESTER UNITED YATAJA UCHOVU KUWA SABABU YA KUCHAPWA MABAO 3-1 FA
MANCHESTER UNITED YATAJA UCHOVU KUWA SABABU YA KUCHAPWA MABAO 3-1 FA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZRzDZrZMDAhCr6znm3M2gBNCOkJu5Salbx_jDkqwo8uStgxP2ws_6obnkdbf-dxGaJndLrovmbvQhiXx91fOpxXnEZTc8xsIuSOQ8rZK7xBsV8NC142updoG2gTuyNlswmTC__Uuml-lC/w640-h430/Leicester+v+United.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZRzDZrZMDAhCr6znm3M2gBNCOkJu5Salbx_jDkqwo8uStgxP2ws_6obnkdbf-dxGaJndLrovmbvQhiXx91fOpxXnEZTc8xsIuSOQ8rZK7xBsV8NC142updoG2gTuyNlswmTC__Uuml-lC/s72-w640-c-h430/Leicester+v+United.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/manchester-united-yataja-uchovu-kuwa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/manchester-united-yataja-uchovu-kuwa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy