ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu FC ya Mbeya mipango yake ya kusepa na pointi sita mbele ya Azam FC msimu wa 2020/21 imekwama kwa kuf...
ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu FC ya Mbeya mipango yake ya kusepa na pointi sita mbele ya Azam FC msimu wa 2020/21 imekwama kwa kufungwa nje ndani.
Mchezo wa kwanza walipokutaba Mbeya, Ihefu ilikubali kichapo cha mabao 2-0 ambapo watupiaji walikuwa ni Ayoub Lyanga na Idd Seleman.
Huo ulikuwa ni mchezo wa Kwanza mwa Katwila baada ya kujiunga na Ihefu akitokea Klabu ya Mtibwa Sugar na jana Machi 11 ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-0.
Mabao yalifungwa na Idd Seleman ambaye alitupia mawili na Lyanga naye alitupia bao moja hivyo Ihefu imefungwa jumla ya mabao matano na kuacha pointi sita mikononi mwa Azam FC.
Matokeo hayo yanaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 44 ikiwa nafasi ya tatu na Ihefu FC ipo nafasi ya 16 na pointi zake ni 20.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS