Hussein Bashe: Mahindi ya Tanzania ni salama kwa afya
HomeHabari

Hussein Bashe: Mahindi ya Tanzania ni salama kwa afya

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema mahindi yanayotoka Tanzania yanakidhi vigezo vya kiafya kinyume na taarifa zinazosambaa kuto...

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema mahindi yanayotoka Tanzania yanakidhi vigezo vya kiafya kinyume na taarifa zinazosambaa kutoka Kenya.

Bashe amesema hayo  kupitia ukurasa wake wa Twitter (@HusseinBashe) na kuongeza kuwa zao hilo kutoka Tanzania linakidhi matakwa ya ndani na nje ya nchi.

“Mahindi ya Tanzania ni salama kwa matumizi ya binadamu na wanyama na yanakidhi vigezo vyote vya kikanda na kimataifa, ameandika.”

Mnamo Machi 5, 2021 Mamlaka ya Kilimo na Chakula, Kenya ilitoa taarifa ya kusitisha mara moja uingizaji wa mahindi kutoka Tanzania na Uganda kwani mahindi kutoka nchi hizo mbili yamepimwa na kuonesha kuwa na sumu zitokanazo na mazao kuliwa na fangasi (sumukuvu).

Naibu Waziri Bashe amesema kuwa wanaendelea na mazungumzo na Kenya kama wanachama wa Umoja wa Afrika Mashariki (EAC) ili kufikia maelewano mazuri.

Aidha, Bashe amesema majibu ya sampuli iliyochukuliwa na Kenya ni tofauti na majibu ya awali ya Shirika la Viwango la Kenya (KEBS).

“Biashara ni suala la hiari, wanaweza kununua au kutonunua kutoka kwetu. Kinachotusumbua sisi ni kauli ya upotoshaji ya Wizara ya Kilimo ya Kenya. Sisi Tanzania tunafanya Biashara ya Mahindi na Mataifa na taasisi za kimataifa na inaendelea,” ameongeza Bashe.

Tanzania inaendelea kuuza mahindi katika nchi za Burundi, DRC, Rwanda na Sudani Kusini.


 


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Hussein Bashe: Mahindi ya Tanzania ni salama kwa afya
Hussein Bashe: Mahindi ya Tanzania ni salama kwa afya
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg1eVvYOSSgsU4BSx0IlIO_hSsV1hTW_u5KfA2awCgv5hu-SmZ19CkRaWOc-xqcpUoSpppC5tpcoWiccbNEx_TtpZVsierscKoH3VXAgcNVknO7aLeEOJ6Wq0Sae0u3ruSP0R9SddYVtt3l/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg1eVvYOSSgsU4BSx0IlIO_hSsV1hTW_u5KfA2awCgv5hu-SmZ19CkRaWOc-xqcpUoSpppC5tpcoWiccbNEx_TtpZVsierscKoH3VXAgcNVknO7aLeEOJ6Wq0Sae0u3ruSP0R9SddYVtt3l/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/hussein-bashe-mahindi-ya-tanzania-ni.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/hussein-bashe-mahindi-ya-tanzania-ni.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy