COSOTA Kusimamia Hakimiliki Ya Sanaa Za Ufundi Katikamfumo Wa Mauzo Kwa Mtandao
HomeHabari

COSOTA Kusimamia Hakimiliki Ya Sanaa Za Ufundi Katikamfumo Wa Mauzo Kwa Mtandao

Anitha Jonas – COSOTA, Dar es Salaam Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa ameagiza COSOTA na BASATA kuan...


Anitha Jonas – COSOTA, Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa ameagiza COSOTA na BASATA kuandaa mfumo wa kuuza kazi za Wachoraji na Wachongaji kwa njia ya mtandao.

Mheshimiwa Bashungwa ametoa agizo hilo jana Jijini Dar es Salaam katika kikao chake na Wasanii wa Sanaa ya Uchoraji na uchongaji nchini kilicholenga kutatua  changamoto Zinazowakabili katika uendeshaji wa kazi zao ikiwemo suala la masoko.

“Katika karne hii ya 21 suala la Masoko linafanyika kwa njia ya mtandao na njia hii ni rahisi na inatangaza biashara kwa haraka zaidi na katika hili COSOTA mtatakiwa kuhakikisha mnalinda Hakimiliki za kazi hizo,”alisema Mhe.Bashungwa.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo Waziri huyo aliwasihi Wachoraji na Wachongaji kusajili kazi zao COSOTA ili ziweze kulindwa, pia alitoa msisitizo kwa wadau hao kuhakikisha wanawasiliana BASATA pamoja na COSOTA pale wanapokuwa na mikataba yao kibiashara kwa lengo la  kupata ushauri wa kisheria ili kuweza  kulinda kazi hiyo pamoja na maslahi yake.

Pamoja na hayo naye Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bibi.Doreen Sinare alieleza kuwa taasisi hiyo imetengeneza Kanuni mpya ambazo zitawasaidia Wachoraji na Wachongaji kunufaika na kazi zao baada ya kuuza kazi zao na kazi hizo kwenda kuuzwa tena nje ya nchi kupitia minada na njia nyingine kama hizo ambapo kazi huuzwa kwa bei za juu ilihali msanii kutokupata chochote  kutokana  na mauzo hayo zijulikanazo kama ‘resale royalties rights’.

“Napenda kuwasisitiza kuhusu suala la kusajili kazi zenu kuna wakati nilitembelea ofisi za Tingatinga na nikawashauri kuhusu suala la kusajili kazi zenu COSOTA lakini baadhi yenu walikuja ila wengine hawakuja sasa naendelea kuwasisitiza kusajili msisubiri mpaka mnapopata changamoto ndiyo mnaanza kuhangaika,”alisema Bibi.Doreen.

Pamoja na hayo Mtendaji huyo alieleza dhamira  yake ya kutembelea eneo la biashara ya vinyago Mwenge Machi 19, 2021 kwa lengo la kuwapa elimu ya Hakimiliki na Hakishiriki ili kuwaongezea uelewa wa masuala hayo ikiwemo maboresho ya Kanuni mbalimbali zinazosimamia hakimiliki.

Pamoja na Kituo cha Wachoraji wa Sanaa ya Tingatinga Oysterbay ambapo itakuwa ni mara nyingine anawatembelea

Mbali na hayo Bibi.Doreen alitangaza  napenda kutoa ofa kwa wanawake wanaofanya kazi ya Sanaa ya Ufundi kupamba Ofisi ya COSOTA kwa kazi zao   ikiwemo kwa Sanaa ya uchoraji au uchongaji

Kufuatia mgogoro wa Tingatinga Arts na Kampuni ya Kenya Mtendaji Mkuu wa COSOTA aliwaelekeza viongozi wa chama hicho  kumpeleka  mkataba wao katika Ofisi yake ili aweze kutoa ushauri.

Pamoja na hayo Katika kikao Waziri Bahungwa alisisitiza mikataba huo ufuatiliwe na COSOTA, na kama kuna haki za Tingatinga basi haki hizo zifuafuatiliwe na zipatikane  hii ni kutokana na sintofahamu ya kusemekana kuwepo kwa baadhi ya wasanii ambao walisaini na kulipwa kwa kazi hiyo. Hivyo mkataba ndio utatoa picha kamili.

Kwa upande Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Bw.Andrian Nyangamale alitoa ombi kwa Serikali kuwa anaomba katika zawadi zile za vinyago au picha za kuchorwa zinazotolewa kwa wageni Ikulu basi Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ataje jina la aliyefanya fanya kazi hiyo pale anapokabishi. *Mh. Waziri alipokea na kuahidi kufanyia kazi jambo hilo


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: COSOTA Kusimamia Hakimiliki Ya Sanaa Za Ufundi Katikamfumo Wa Mauzo Kwa Mtandao
COSOTA Kusimamia Hakimiliki Ya Sanaa Za Ufundi Katikamfumo Wa Mauzo Kwa Mtandao
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjjfi36UPXYCf6W0x7udyslZ-dpa3DcsRnEPlo97kxSchKEkzpW6C6NulOeb9cKmJkfkcEZUwhihIgOlc1PvIFbz4GoIhF-eC3VFe3atR5_xX8X5GyzekuP5_d8RtUuiAPoA6eLsTRVD7xJ/s16000/1.jpeg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjjfi36UPXYCf6W0x7udyslZ-dpa3DcsRnEPlo97kxSchKEkzpW6C6NulOeb9cKmJkfkcEZUwhihIgOlc1PvIFbz4GoIhF-eC3VFe3atR5_xX8X5GyzekuP5_d8RtUuiAPoA6eLsTRVD7xJ/s72-c/1.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/cosota-kusimamia-hakimiliki-ya-sanaa-za.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/cosota-kusimamia-hakimiliki-ya-sanaa-za.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy