KUELEKEA kwenye mchezo wa leo Machi 16, Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi kati ya Simba dhidi ya Al Merrikh, Kocha Mkuu wa wapinz...
KUELEKEA kwenye mchezo wa leo Machi 16, Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi kati ya Simba dhidi ya Al Merrikh, Kocha Mkuu wa wapinzani wa Simba, Lee Clark amesema kuwa vijana wake wapo tayari kupata ushindi leo.
Mchezo wa leo kwa Simba utakuwa na ushindani mkubwa kwa sababu Al Merrikh inahitaji kufufua matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali huku Simba nao wakihitaji nafasi hiyo.
Kundi A kwa sasa halina mwenyewe kwa kuwa kinara Simba ana pointi 7, AS Vita na Al Ahly wana pointi nne huku Al Merrikh akiwa na pointi moja kwa namna yoyote akishinda matumaini yanarejea.
Clark amesema: "Maandalizi ni mazuri na tupo tayari vijana wanahitaji ushindi hakuna lingine,".
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS