ZIDANE:NGUVU KUBWA NA KUJILINDA SABABU YA USHINDI
HomeMichezo

ZIDANE:NGUVU KUBWA NA KUJILINDA SABABU YA USHINDI

  KOCHA Mkuu wa Klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kuwa sababu kubwa ya timu yake kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Atlanta k...

 


KOCHA Mkuu wa Klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kuwa sababu kubwa ya timu yake kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Atlanta kwenye mchezo wao uliochezwa Februari 24 ni utimamu wa mwili wa wachezaji wake pamoja na matumizi ya nguvu.


Zidane amesema:-“Wachezaji walikuwa timamu sana kimwili na matumizi makubwa ya nguvu jambo ambalo limeweza kuwapa ushindi ndani ya uwanja.

 "Pia jambo jingine ilikuwa ni kuweza kuongeza nguvu kwa upande wa kujilinda hilo nalo ni muhimu kwao hivyo wanastahili pongezi,".


Ni mchezaji wao Remo Freuler dakika ya 17 alionyeshwa kadi nyekundu na kuwafanya Atlanta kumaliza wakiwa pungufu kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Atletti Azzurri d'italia.

 Kwa upande wa kocha wa Atalanta, Giann Piero Gasperini ameoneshwa kutokufurahishwa na matokeo hayo kwani yalikuwa nje ya matarajio yao. 


“Nimesikitishwa kwa kutoweza kuucheza mchezo kama tulivyotaka. Ulikuwa mchezo tofauti baada ya kuwa pungufu. Tukapaswa kujilinda zaidi.

 

 “Tunapaswa kushinda kwenye mchezo wa marudiano Madrid, ni rahisi hatupaswi kufikiria sana. Tuna uwezekano mmoja tu, tunapaswa kushinda”.

 

Atalanta ina kazi nyingine tena Machi 16 mwaka huu wakati watakapokutana tena na Real Madrid nchini Hispania kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa hatua hiyo ya 16 bora ya michuano hiyo.

 Ni beki wa kushoto wa Real Madrid, Ferland Mendy alipachika bao la ushindi kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya.

 Mendy alifunga bao hilo dakika nne kabla mchezo kumalizika baada ya kupokea pasi ya Luka Modric akiwa nje ya eneo la 18 na kupiga mpira kwa ustadi mkubwa uliomshinda mlinda mlango wa Atalanta, Pierluigi Golini na kutinga wavuni.

 

Bao hilo ni kwanza kwa Mendy aliyecheza michezo 20 kwenye michuano hiyo pekee, ilhali ni la pili kwenye michezo 22 aliyecheza kwenye michuano yote msimu huu akiwa na miamba hiyo ya soka kutoka nchini Hispania.

 


Kwa upande wa rekodi, Real Madrid imepata ushindi wake wa kwanza kwa Atalanta, kwani wawili hao walikuwa wanakutana kwa mara yao ya kwanza huku Atalanta ikiweka rekodi ya kucheza mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza bila kupiga shuti hata moja lililolenga lango




Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: ZIDANE:NGUVU KUBWA NA KUJILINDA SABABU YA USHINDI
ZIDANE:NGUVU KUBWA NA KUJILINDA SABABU YA USHINDI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiggBqc_OktcxEymFIsz5DI5b61eX4P9fbi__MEGcl9C4lDwCeSjylbsrlHwvwqhemGBO5WxGOw3lCcAArucCi-pB9K5PfYCuzbCMaB_PDvc_FOjfhNFCKA27pW4eKpeP0wsFPpDD2Mbgci/w640-h366/Mendy+sasa.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiggBqc_OktcxEymFIsz5DI5b61eX4P9fbi__MEGcl9C4lDwCeSjylbsrlHwvwqhemGBO5WxGOw3lCcAArucCi-pB9K5PfYCuzbCMaB_PDvc_FOjfhNFCKA27pW4eKpeP0wsFPpDD2Mbgci/s72-w640-c-h366/Mendy+sasa.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/zidanenguvu-kubwa-na-kujilinda-sababu.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/zidanenguvu-kubwa-na-kujilinda-sababu.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy