Waziri Lukuvi Aagiza Wenyeviti Wa Mabaraza Ya Ardhi Kuanza Kutumia Lugha Ya Kiswahili
HomeHabari

Waziri Lukuvi Aagiza Wenyeviti Wa Mabaraza Ya Ardhi Kuanza Kutumia Lugha Ya Kiswahili

Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewaagiza Wenyeviti wa Mabaraza ya ardhi n...


Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewaagiza Wenyeviti wa Mabaraza ya ardhi na Nyumba ya wilaya kutumia lugha ya Kiswahili katika kuandika hukumu.

Lukuvi alitoa maagizo hayo tarehe 5 Februari 2021 jijini Dodoma alipozungumza na Wenyeviti pamoja na Wasajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kwa nchi nzima kupitia Video (Video conference).

‘’Nasisitiza wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya mtumie lugha ya Kiswahili wakati wa kuandika hukumu zenu kama alivyoagiza mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli na nitashangaa kumuona mwenyekiti akiandika hukumu kwa lugha ya kiswahili’’ alisema Lukuvi

Aidha, Lukuvi aliwataka pia wenyeviti hao wa Mabaraza kuchapa hukumu za maamuzi wanayotoa wao wenyewe bila kutegemea Makarani na hukumu hizo zitoke kwa wakati na kusisitiza kuwa katika dunia ya leo suala la uzembe halina nafasi.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliongeza kwa kusema kuwa, pamoja na kuwepo uchache wa watumishi kwenye baadhi ya ofisi za Mabaraza ya Ardhi lakini watendaji hao wanatakiwa kuwajibika na kuacha visingizio pamoja na kufanya kazi kwa mazoea kwa kuwa serikali iko katika juhudi za kuhakikisha inajaza nafasi.

Kwa mujibu wa Lukuvi, hivi sasa ni wajibu wa watendaji wa mabaraza ya ardhi kufanya kilicho sahihi na kuwa wabunifu sambamba  na kuwajibika kwa kutoa hukumu kwa wakati  na kusisitiza wananchi masikini wanategemea sana matumizi ya Kiswahili.

‘’Maamuzi yetu kama wenyeviti wa Mabaraza yawe rahisi na sisi tuwe wa kwanza kuwasaidia wananchi na kila mwenyekiti atekeleze maamuzi haya kwa lugha ya Kiswahili’’ alisema Lukuvi

Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, wapo wananchi waliokosa haki zao ama kuchelewa kukata rufaa kutokana na kutokujua kilichoandikwa katika hukumu kwa kuwa kimeandikwa kwa kiingereza.

Kwa upande wake Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Stella Tullo aliwataka Wenyeviti wa Mabaraza kuanza kutekeleza maagizo ya Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mapema kwa kuzingatia sheria na taratibu.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Lukuvi Aagiza Wenyeviti Wa Mabaraza Ya Ardhi Kuanza Kutumia Lugha Ya Kiswahili
Waziri Lukuvi Aagiza Wenyeviti Wa Mabaraza Ya Ardhi Kuanza Kutumia Lugha Ya Kiswahili
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiM4_mJoxeQluXovXj2mZR_STPjkqQ-xgj7fy5asN9xikf26mwTKdUl88RRCxRGmuXc04s8NHlrfASmDkVkzTxw4-vXx8FacMQnngRDOdBbzXoWhyA1TLQkDotifmM8iXzra3D4e70DPI7_/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiM4_mJoxeQluXovXj2mZR_STPjkqQ-xgj7fy5asN9xikf26mwTKdUl88RRCxRGmuXc04s8NHlrfASmDkVkzTxw4-vXx8FacMQnngRDOdBbzXoWhyA1TLQkDotifmM8iXzra3D4e70DPI7_/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/waziri-lukuvi-aagiza-wenyeviti-wa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/waziri-lukuvi-aagiza-wenyeviti-wa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy