WAPINZANI wa Simba kwenye mchezo ujao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, Al Ahly ya Misri wameanza kwa ushindi wa mabao 3...
WAPINZANI wa Simba kwenye mchezo ujao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, Al Ahly ya Misri wameanza kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Al Merrik.
Mabao ya Al Ahly yalipachikwa na Mohamed Magdy dakika ya 57, Kahraba dakika ya 63 na Walter Bwalya dakika ya 71, Uwanja wa Cairo.
Ushindi huo unawafanya kwa sasa Al Ahly wawe vinara wa kundi A ambalo awali lilikuwa linaongozwa na Simba baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS Vita kwenye mchezo waliocheza ugenini.
Wanatarajiwa kukutana na Simba iliyo nafasi ya pili ila ina pointi tatu na bao moja Februari 23, kwenye mchezo wa hatua ya makundi Uwanja wa Mkapa.
Kwenye mchezo huo wakati wakishinda mabao hayo na kuonyesha balaa ndani ya uwanja, Al Ahly walipiga jumla ya mashuti 22 langoni kwa wapinzani wao Al Merrikh na katika hayo ni mashuti 6 yalilenga lango huku wapinzani wao walipiga jumla ya mashuti 8 na katika hayo manne yalilenga lango.
Umiliki wa mpira Al Ahly ilikuwa ni asilimia 71 na wapinzani wao asilimia 29 na walipiga jumla ya pasi 648 huku Al Merrikh walipiga jumla ya pasi 272 hivyo Simba wana kazi ya kufanya ndani ya kundi A.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS