UONGOZI wa Mtibwa Sugar umeweka wazi kwamba leo utawafunga Yanga kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, saa 1:0...
UONGOZI wa Mtibwa Sugar umeweka wazi kwamba leo utawafunga Yanga kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, saa 1:00 usiku hivyo wajipange kisaikolojia kuyakubali matokeo hayo.
Yanga inakumbuka kwamba iliwafunga Mtibwa Sugar bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro bao lilifungwa na Lamine Moro.
Leo inakutana na Mtibwa Sugar ambayo imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Ihefu, Uwanja wa Jamhuri na Yanga wenyewe wametoka kulazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Mkapa.
Thobias Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa mafunzo ambayo wamepewa wachezaji wake chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery wanaamini yatawapa matokeo mazuri na watashinda mbele ya Yanga.
Kwa sasa nyota wao Dickson Job ambaye alikuwa anacheza ndani ya Mtibwa Sugar ameanza maisha mapya ndani ya Yanga.
Hatakutana na waajiri wake wa zamani kwa kuwa anasumbuliwa na nyama za paja ila tayari ameanza mazoezi mepesi.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS