Mameneja Na Wahandisi Wakuu Wasimamishwa Kazi
HomeHabari

Mameneja Na Wahandisi Wakuu Wasimamishwa Kazi

Na Zuena Msuya Dar es Salaam, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametaka Meneja wa Kituo cha Kupoza na Kusambaza umeme cha Kinyerez...

Breaking: NECTA Yatangaza Matokeo ya Kidato cha Nne, Darasa la Nne, Kidato cha pili
Taarifa kwa Umma Toka Idara ya Uhamiaji
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo January 15


Na Zuena Msuya Dar es Salaam,
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametaka Meneja wa Kituo cha Kupoza na Kusambaza umeme cha Kinyerezi I, Ubungo I pamoja na Mhandisi Mkuu wa Kinyerezi II, Kinyerezi I, na Ubungo I, wasimamishwe kazi na wachunguzwe kwa uzembe.

Dkt. Kalemani ametoa maagizo hayo, wakati wa ziara yake ya kukagua vituo hivyo na baadaye kuzungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Februari 06, Jijini Dar es Salaam.

Aidha alitoa siku kumi na nne (14) kwa Bodi hiyo kuwafanyia uchunguzi mameneja na wahandisi wakuu hao na kumpatia majibu stahiki Waziri wa Nishati.

Dkt. Kalemani alisema kuwa, alifanya maamuzi hayo baada ya kubaini uzembe uliofanyika katika vituo hivyo, ikiwemo kutokuwepo kazini kwa watendaji hao na kutowajibika ipasavyo katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.

“Haiwezekani Meneja na Mhandisi Mkuu wote wasiwepo katika vituo vyenu vya kazi bila sababu za msingi, mitambo yote inafanyiwa ukarabati kwa wakati mmoja! Hapana, hii haiwezekani ni uzembe wa hali ya juu lazima wachunguze na waondoe katika nafasi zao za kazi hawa watu wasije kutuletea matatizo”, alisema Dkt. Kalemani.

Aidha aliiagiza Bodi ya TANESCO, kuhakikisha kuwa, mtaalamu wa kuunga kifaa cha kubusti umeme kilichopata hitilafu katika Kituo cha Kupoza umeme cha Kinyerenzi I, anapatikana na kufunga kifaa hicho ndani ya siku tatu (3) kuanzia leo na kituo hicho kizalishe umeme kama ilivyokuwa hapo awali.

Sambamba na hilo, aliwataka wataalamu wanaofanya ukarabati katika vituo hivyo kufanya kazi hiyo usiku na mchana ili kukamilisha matengenezo hayo haraka, ili kuruhusu vituo hivyo kuzalisha umeme wote unaotakiwa katika kituo husika.

Vilevile aliitaka Bodi hiyo kufanya ukaguzi katika vituo vya kupoza na kusambaza umeme ili kuona hali halisi ya uzalishaji wa umeme katika mitambo yote, na ndani ya kipindi cha miezi miwili (2) mitambo yote tisa (9) iwe inafanya kazi kwa ufanisi.

“Bodi muanze kufanya uchunguzi kwa wataalamu wanaosimamia mitambo ya umeme, na endapo mtabaini asiyemuaminifu na anayekwenda kinyume na maadili yake ya kazi, lazima achukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu mapema hata kabla ya wizara kuingilia kati”, alisisitiza Dkt. Kalemani.

Katika hatua nyingine, aliwataka Mameneja TANESCO katika maeneo ya Chanika, Gongolamboto,Pugu na ukanda mzima wa maeneo hayo waeleze sababu ya kukatika kwa umeme katika maeneo hao mara kwa mara hali ya kuwa hakuna mgao na umeme upo mwingi wakutosha na ziada.

Alieleza wazi kuwa, endapo mameneja hao wameshindwa kutatua tatizo hilo ni dhahiri wameshindwa kufanya kazi, hivyo waondolewe katika nafasi hizo na wawekwe wale wenye uwezo wa kuwahudumia wananchi.

Akizungumzia suala la upatikanaji wa umeme nchini, Dkt. Kalemani alisema kuwa, hataki kusikia malalamiko ya wananchi kukosa umeme kwa sababu ya mitambo kuharibika, pia kuwaunganishia huduma ya umeme wale wote ambao wamekwisha lipia huduma hiyo kwa kuwa vifaa vipo vya kutosha, umeme upo mwingi na wakutosha.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mameneja Na Wahandisi Wakuu Wasimamishwa Kazi
Mameneja Na Wahandisi Wakuu Wasimamishwa Kazi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEigMklXrSAjM82LJgih2rUXMTY53ZHWS0uU16cE7XShTn58iuExKVi1elquXHdUbDmZy-0rXPwd8sD9jJdN5vEFPf6NCCppdJMmpniVW3BZEEmF8hLsjsiiQFpeGOv5qGOChz2gUzTBkEIQ/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEigMklXrSAjM82LJgih2rUXMTY53ZHWS0uU16cE7XShTn58iuExKVi1elquXHdUbDmZy-0rXPwd8sD9jJdN5vEFPf6NCCppdJMmpniVW3BZEEmF8hLsjsiiQFpeGOv5qGOChz2gUzTBkEIQ/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/mameneja-na-wahandisi-wakuu.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/mameneja-na-wahandisi-wakuu.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy