KOCHA YANGA: SIMBA IONGEZE NGUVU SAFU YA ULINZI KIMATAIFA
HomeMichezo

KOCHA YANGA: SIMBA IONGEZE NGUVU SAFU YA ULINZI KIMATAIFA

  MOHAMED Hussein,’Mmachinga’ kocha msaidizi ndani ya timu ya Yanga Princes amesema kuwa wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa A...


 MOHAMED Hussein,’Mmachinga’ kocha msaidizi ndani ya timu ya Yanga Princes amesema kuwa wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika lazima waongeze nguvu kwenye safu ya ulinzi ambayo inafanya makosa mara kwa mara.

Mmachinga alikuwa ni mchezaji wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania ni miongoni mwa Legendi ambao waliweka rekodi kwenye soka la Bongo kutokana na uwezo wake wa kucheka na nyavu.


Simba ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa imecheza jumla ya mechi 18, safu ya ulinzi imeruhusu mabao 8 yaliyookotwa nyavuni na safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 42.

Ina kazi ya kumenyana na AL Ahly ya Misri, Februari 23 baada ya kumalizana na AS Vita ya Congo,Februari 12 kwa ushindi wa bao 1-0 ambao ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya makundi.

Mmachinga amesema:”Kwa upande wa ushambuliaji na viungo kidogo Simba imeimarika ila shida ipo kwenye ulinzi hapo ndipo ambapo panahitaji umakini mkubwa na kuongeza nguvu katika kuweka ulinzi.

"Kwenye mashindano ya kimataifa wanakutana na aina tofauti ya washambuliaji, kwenye mechi za kimataifa washambuliaji wana mbinu nyingi na uwezo wa kutumia nafasi.

"Ikiwa wataongeza nguvu kwenye safu yao ya ulinzi itawafanya wawe na uimara wa kumiliki mpira na kupunguza hatari," amesema.

Kipa namba moja Aishi Manula kwenye mchezo dhidi ya AS Vita ya Congo aliokoa hatari tano ambazo ziliwapita walinzi wa Simba jambo lililofanya viungo pamoja na wahsambuliaji kuungana na safu ya ulinzi inayoongozwa na Joash Onyango pamoja na Pascal Wawa.



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: KOCHA YANGA: SIMBA IONGEZE NGUVU SAFU YA ULINZI KIMATAIFA
KOCHA YANGA: SIMBA IONGEZE NGUVU SAFU YA ULINZI KIMATAIFA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhNQPdRLLedhyphenhyphenBRmpf94hrfeDtjmBuEZ81EBmij4jtsz1axYPtvCU6wm97eoKuqayIs-BNaSDMfGXSGlVGjmLzky9qumMbUE7se57X7QS_z8ZyZNj-2br0FhXkiofy4yusmERY07DcG6_tR/w640-h542/Onyango+Simba.PNG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhNQPdRLLedhyphenhyphenBRmpf94hrfeDtjmBuEZ81EBmij4jtsz1axYPtvCU6wm97eoKuqayIs-BNaSDMfGXSGlVGjmLzky9qumMbUE7se57X7QS_z8ZyZNj-2br0FhXkiofy4yusmERY07DcG6_tR/s72-w640-c-h542/Onyango+Simba.PNG
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/kocha-yanga-simba-iongeze-nguvu-safu-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/kocha-yanga-simba-iongeze-nguvu-safu-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy