UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa utapambana kusaka ushindi kwenye mechi zao ambazo zimebaki ili kurejea kwenye ubora. Kikosi hicho ki...
UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa utapambana kusaka ushindi kwenye mechi zao ambazo zimebaki ili kurejea kwenye ubora.
Kikosi hicho kinanolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ambaye amerithi mikoba ya Aristica Cioaba aliyechimbishwa ndani ya kikosi hicho kutokana na kile kilichoelezwa kuwa mwendo mbovu wa timu hiyo.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wanatambua kwamba mashabiki wanahitaji ushindi hivyo wanaamini kuwa watapata matokeo chanya kwenye mechi zao.
"Tupo imara kwani kushindwa kupata matokeo kwenye mechi zetu haina maana kwamba hatupo imara tutafanya vema na tutarudi kwenye ubora.
"Kinachotokea ndani ya uwanja ni matokeo ila hakuna kibaya ndani ya uwanja, wachezaji wana morali na wanapenda kufanya kazi yao ni suala la muda,".
Mchezo uliopita Azam FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union, uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga na ingizo jipya,Mpiana Monzinzi.
Azam FC kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya 3 ikiwa imecheza jumla ya mechi 19 na kukusanya pointi 33.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS