Ipo Haja Ya Kuzijengea Uwezo Halmashauri Zote Nchini-Waziri Ummy
HomeHabari

Ipo Haja Ya Kuzijengea Uwezo Halmashauri Zote Nchini-Waziri Ummy

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu amesema ipo haja ya kuzijengea uwezo halmashauri zote nc...


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu amesema ipo haja ya kuzijengea uwezo halmashauri zote nchini ili ziweze kuwa na usimamizi mzuri wa taka katika madampo.

Ummy amesema hayo Januari 27, 2020 wakati akiwasilisha Taarifa kuhusu muundo wa Ofisi ya Makamu wa Rais na Utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo inayosimamia utekelezaji wa majukumu ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira katika Ofisi za Bunge jijini Dodoma.

Alisema kuwa kumekuwepo na changamoto ya kutokuwepo na usimamizi mzuri wa taka zinazotupwa katika madampo na badala yake zinaachwa na kurudi kwenye makazi ya watu hali inayohatarisha afya zao.

‘’Halmashauri zikifanya sorting (kutenganisha) aina za taka kwa mfano chupa za plastiki zinapelekwa viwandani kurejelezwa, taka za mabaki ya chakula zinafanya kuwa mbolea tutakuwa tumefanikiwa kusimamia na kudhibiti taka kwenye madampo,” alisema Ummy.

Alitaja mikakati itakayokelezwa kuwa ni pamoja na kuhamasisha usimamizi na udhibiti wa taka kwa kutumia dhana ya Punguza, Tumia tena na Rejeleza kwa lengo kupunguza gharama za usimamizi na udhibiti wa taka katika mamlaka za Serikali za Mitaa.

Pia waziri huyo alisema Serikali itaimarisha usimamizi na hifadhi ya mazingira kwa ajili ya maendeleo endelevu pamoja na uratibu na utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Mazingira.

Kwa upande mwingine Waziri Umya alibanisha kuwa upo utegemezi mkubwa wa matumizi ya mkaa na kuni kama chanzo cha nishati ya kupikia pamoja na shughuli za kilimo zisizo endelevu jail inayosababisha ongezeko la uharibifu wa mazingira nchini.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau imeendelea kuhamasisha kampeni ya upandaji miti, matumizi ya nishati mbadala kama gesi na kuweka mikakati ya uhamasishaji wa kilimo kinachozingatia uhifadhi wa mazingira.

Aliongeza kuwa Serikali imeweka mikakati ya kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala kwa ajili ya kupikia katika ngazi ya kaya na taasisi za umma na binafsi hususan taasisi za elimu na mafunzo, Magereza, na Majeshi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. David Kihenzile alipongeza kampeni ya Serikali kupitia Ofisi hiyo ya kupanda na miti ambapo alishauri kuwe na mikakati ya kuwa na takwimu za miti inayostawi.

Pia Kihenzile alipendekeza kuwepo na mkakati wa kujenga madampo ya kisasa katika wilaya zote ili kuweza kudhibiti taka na kuyafanya maeneo hayo kuwa masafi.

‘’Ningependekeza tuwe na mikakati kabambe ya kupanda miti na tunaweza kuwa na mkakati maalumu kwa Jiji hili la Dodoma ambalo kwa sasa ndio makao makuu ya nchi,” alishauri Kihenzile.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Ipo Haja Ya Kuzijengea Uwezo Halmashauri Zote Nchini-Waziri Ummy
Ipo Haja Ya Kuzijengea Uwezo Halmashauri Zote Nchini-Waziri Ummy
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiC4SaDID1F2WHImkQv32V5DScqN-5s0844kllygIxjs4I9hkac4j3z6Z8__Tt4QZ_JeCUuJSAbByEvUz_O57rfcY9VaUJQ-siCUnSgpQNvVaB5iTx1uDreUdEhZUyVFDru-jImvbH6qELN/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiC4SaDID1F2WHImkQv32V5DScqN-5s0844kllygIxjs4I9hkac4j3z6Z8__Tt4QZ_JeCUuJSAbByEvUz_O57rfcY9VaUJQ-siCUnSgpQNvVaB5iTx1uDreUdEhZUyVFDru-jImvbH6qELN/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/01/ipo-haja-ya-kuzijengea-uwezo.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/01/ipo-haja-ya-kuzijengea-uwezo.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy