Lowassa, Majaliwa kuhudhuria kuingizwa kazini kwa Dk Shoo
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.     
HomeHabariKitaifa

Lowassa, Majaliwa kuhudhuria kuingizwa kazini kwa Dk Shoo

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.      Moshi. Maaskofu zaidi ya 30 kutoka ndani ya nje ya nchi, leo wanatarajiwa kuhudhu...

Chama cha ACT chamwandalia Zitto makazi >>>Soma yote hapa
Simba Yagongwa Virungu viwili na Mgambo, Ivo alambwa kadi Nyekundu
Ukawa wagawana Majimbo 211


Moshi. Maaskofu zaidi ya 30 kutoka ndani ya nje ya nchi, leo wanatarajiwa kuhudhuria tukio la kuingizwa kazini kwa Mkuu mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk Fredrick Shoo.

Miongoni mwa maaskofu hao ni pamoja na 24 wa dayosisi zote za KKKT, maaskofu wa lutherani kutoka mataifa mbalimbali duniani na maaskofu wa makanisa rafiki.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tukio hilo litakalofanyika katika Usharika wa Moshi na aliwasili mjini hapa jana.

Pia tukio hilo litashuhudiwa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, wabunge na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ambaye pia ni Mkuu wa Pili wa Jimbo Kilimanjaro Kati la KKKT, Mchungaji Fred Njama aliliambia gazeti hili kuwa, viongozi mbalimbali wamethibitisha kushiriki.

Kulingana na ratiba iliyotolewa, Dk Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ataingizwa kazini katika ibada itakayoendeshwa na Mkuu wa KKKT mstaafu, Dk Alex Malasusa.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala aliwaambia waandishi wa habari juzi kuwa, Majaliwa angewasili na tukio linalomleta ni la sherehe hizo.

Dk Shoo alichaguliwa kuwa mkuu wa kanisa hilo katika mkutano mkuu wa 19 wa KKKT uliofanyika Agosti 14, mwaka jana na atatumikia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka minne.

Katika mkutano wa uchaguzi askofu huyo alipata kura 153 dhidi ya 67 za Askofu Dk Stephen Munga wa Dayosisi ya Kaskazini ambaye alichuana naye katika duru ya pili. 

Chanzo: Mwananchi
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Lowassa, Majaliwa kuhudhuria kuingizwa kazini kwa Dk Shoo
Lowassa, Majaliwa kuhudhuria kuingizwa kazini kwa Dk Shoo
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg-SYPx_YYLFkOjDoNxn1JwNziS0qHxm4W72EiCDY39EeOutQTAgVjMhjkq05Ccm2LloRCeOHCIFqD5Mrr7pMVlAd1BAfma9sPeZ0p3lUMMrBjNRk5rCguLJFbutnRKfyx6UsyrWAYa2YDO/s640/PIC%252BLOWASSA.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg-SYPx_YYLFkOjDoNxn1JwNziS0qHxm4W72EiCDY39EeOutQTAgVjMhjkq05Ccm2LloRCeOHCIFqD5Mrr7pMVlAd1BAfma9sPeZ0p3lUMMrBjNRk5rCguLJFbutnRKfyx6UsyrWAYa2YDO/s72-c/PIC%252BLOWASSA.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2016/01/lowassa-majaliwa-kuhudhuria-kuingizwa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2016/01/lowassa-majaliwa-kuhudhuria-kuingizwa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy