HATIMAYE! I le siku iliyokuwa ikisubiriwa na mashabiki wengi wa burudani imewadia ambapo kesho Aprili, 5 (Sikukuu ya...
HATIMAYE! Ile
siku iliyokuwa ikisubiriwa na mashabiki wengi wa burudani imewadia
ambapo kesho Aprili, 5 (Sikukuu ya Pasaka) ndani ya Uwanja wa Taifa wa
Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar mastaa wa muziki
Bongo kama, Ali Kiba ‘Mwana Dar Live’, Isha Mashauzi pamoja na Msaga
Sumu wanatarajiwa kutikisa.
Akizungumza
na Mikito Nusunusu, mratibu wa burudani katika ukumbi huo, Abdallah
Mrisho ‘Abby Cool’ alianza kwa kuwaomba mashabiki wote kufika kwa wingi
kujionea mastaa hao wakifanya maajabu jukwaani.
“Moto wa burudani utawaka kesho hivyo niwaombe tena, siku ya kesho si ya kukosa kutokana na burudani tulizowaandalia,” alisema Abby Cool.

ALI KIBA
Ikumbukwe kuwa tangu mwaka 2013, Ali Kiba hajafanya shoo yoyote katika ukumbi huo na kwa mara nyingine anakuja kama Mwana Dar Live kutokana na wimbo wake unaotikisa kwa sasa wa Mwana.
“Kwa mara ya kwanza Dar Live, Ali Kiba ataimba nyimbo zake live kwa kutumia vyombo na hii itakuwa mwanzo mwisho hivyo itakuwa burudani ya aina yake.

“Kikubwa
kitakachoamsha shangwe kwa mashabiki ni staili yake mpya atakayoizindua
ya Chekecha Cheketua inayotokana na wimbo wake wenye jina hilohilo huku
akiwa na madensa wake wapya.”
Mbali na kuwepo kwa sapraizi kibao hiyo kesho, mashabiki pia wajiandae kuonjeshwa ngoma zinazobamba alizofanya na mdogo wake wakiwa kama Kiba Square ambazo ni Kidela, Pita Mbele na nyingine nyingi.

ISHA MASHAUZI
Kiongozi wa kundi la muziki wa Pwani, Mashauzi Classic, Isha Mashauzi ‘Jike la Simba’ naye atakuwepo kesho kuwapa burudani mashabiki wote wa muziki huo.“Kwa mara ya kwanza Isha atautambulisha wimbo wake wa Nimpe Nani huku Mashauzi Classic wakiwakonga kwa nyimbo zao kali kama Ropokeni Yanawahusu , Ni Mapenzi Tu, Tupendane, Bonge la Bwana na nyingine nyingi.”

Mashauzi
pia watatoa sapraizi kubwa ikiwa ni pamoja na kuachia nyimbo zao tatu
kwa mpigo ambazo ni Tuacheni Tulale, Mapenzi Yamenivuruga pamoja na Wema
Hauwezi.
PAM D Burudani
pia itafunikwa na msanii anayekuja kwa kasi, Pamela Daffa ‘Pam D’
ambapo kesho anatarajiwa kutoa shoo ya aina yake akiwa sambamba na
madensa wake.Pam D atawabamba na ngoma yake ya Nimempata aliyoshirikiana
na Mesen Selekta ambayo ni habari ya mjini kwa sasa.
MASAI WARRIORS
Mapema kuanzia asubuhi hadi jioni kutakuwa na kundi maarufu la Masai Warriors ambalo litatoa burudani kibao kwa watoto kama vile kucheza na magunia, sarakasi, yoga, kuimba, kugawa zawadi na vingine vingi.
“Niwaombe tu wazazi wawaruhusu watoto wao kuja sehemu hii muhimu kwa burudani za kijanja. Tumewaandalia pia michezo mingi kama vile ya kubembea, kuteleza,kuogelea na kila mmoja atahakikisha anarudi na zawadi nyumbani kemkemu,” alisema Abby.

MSAGA SUMU
Pazia la burudani kwa watu wakubwa litafunguliwa usiku ambapo kwa watu wote watakaofika mapema watapata fursa ya kupiga picha ‘red carpet’ na mastaa wote watakaofika kesho sambamba na kuongea nao machache.

“Kwa mara ya kwanza atazindua nyimbo zake tatu kwa mpigo ambazo ni Marafiki Gani, Shemeji Unanitega pamoja na Kidole Changu.”
COMMENTS