Ngassa akijaribu kumpita mlinzi wa Uganda cranes Shirikisho la mpira Barani Afrika jana lilipanga ratiba ya awali y...
Ngassa akijaribu kumpita mlinzi wa Uganda cranes
Shirikisho la mpira Barani Afrika jana lilipanga ratiba ya awali ya kufuzu katika fainali za mataifa ya Afrika CHAN ya mwaka 2016, ambapo mabingwa wa kombe hilo Libya wamepangwa kukutana na majirani zao Morocco huku Ivory Coast ikiwekwa kundi moja na wapinzani wao Ghana.
CAF imepanga droo hiyo kulingana na kanda za mataifa hayo,Kwa ujumla mashindano hayo yanajumhisha mataifa 42 ambapo yatatoa timu 15 ambazo zitaungana na mwenyeji wa fainali hizo Rwanda kuanza kipute hicho tarehe 16 Januari hadi February 7 mwaka ujao.
Katika kanda ya Afrika Mashariki Burundi imepangwa kupambana dhidi ya Djibouti, Uganda itapambana dhidi ya Tanzania, Kenya dhidi ya Ethiopia wakati Sudan itacheza na timu ambayo itaibuka mshindi katika kundi hilo.
Kanda ya kusini Zimbabwe itapambana dhidi ya visiwa vya Comoro, Lesotho dhidi ya Botswana, Namibia itacheza dhidi ya Zambia kwenye raundi itakayofuata, Mozambique dhidi ya Seychelles, South Afrika dhidi ya Mauritius wakati Swaziland itakutana na Angola.
Kanda ya kati Cameroon itampambana dhidi ya Congo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itakutana na Afrika ya Kati wakati Chad itakutana na Gabon.
Kanda ya Magharibi imegawanyika katika sehemu mbili A na B, kwahiyo kwenye kundi A kuna timu za Guinea-Bissau ambayo itakutana na Mali, Mauritania dhidi ya Sierra Leone wakati Equatorial Guinea itapambana dhidi ya Liberia na Gambia itasubiri kuangalia kama Senegal itaruhusiwa kushiriki mashindano hayo.
Kundi B kuna timu za Nigeria,Burkina Faso, Niger, Togo, katika kundi hilo Nigeria itapambana na Burkina Faso na Togo ikipambana dhidi ya Niger.
Je unaipa nafasi gani Tanzania katika mashindano hayo???
COMMENTS