MUIGIZAJI nyota wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’, amedaiwa kumsaliti mpenzi wake wa siku nyingi, Chuchu Hans baada ya kukutwa akiw...
MUIGIZAJI nyota wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’, amedaiwa kumsaliti mpenzi wake wa siku nyingi, Chuchu Hans baada ya kukutwa akiwa amepozi kimahaba na mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2011, Husna Maulid katika Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar, hivi karibuni.
Wawili
hao waliokuwa wamepakatana, walikutwa katika ukumbi huo wakati bendi
mbili kubwa za muziki wa dansi nchini, FM Academia na The African Stars
‘Twanga Pepeta’ zilipokuwa zikiangusha burudani kabambe ya kushindana.
Uwepo
wa Ray na Husna ulitafsiriwa kuwa ni usaliti kwani muda wote waliokuwa
ndani ya ukumbi huo wawili hao walikuwa wamegandana kimahaba huku
wataalamu wa ubuyu wakikazia madai kwa kusema wawili hao ni wapenzi.
“Sasa
wewe kusoma hujui hata picha huoni? Hawa watakuwa ni wapenzi tu,
haiwezekani mtu mpakatane, mpeane kampani kiasi hiki na mtu ambaye siyo
mtu wako,” alisikika shuhuda mmoja.
Ray
ambaye kabla ya kuwa na Chuchu aliwahi kutoka kimapenzi na mwigizaji
Blandina Changula ‘Johari’ na Ruth Suka ‘Mainda’, alionekana kufurahia
kumpakata Husna huku wakipeana kampani ya kuzungumza, lakini alipatwa na
mshtuko mkubwa baada ya kugundua kuwa alikuwa akifuatiliwa na kamera ya
paparazi wetu.
Kutokana
na mazingira ya wawili hao ukumbini hapo, paparazi wetu alishindwa
kuzungumza nao juu ya ishu hiyo na hata alipowatafuta kwa simu siku
iliyofuata, simu zao ziliita bila kupokelewa (huenda walijua wataulizwa
nini).Lakini Chuchu, ambaye ndiye ‘mmiliki’ wa Ray hivi sasa,
alipoulizwa kama anajua lolote juu ya ukaribu wa watu hao, alishtuka na
kudai haamini kama Ray anaweza kumsaliti au amewahi kupiga picha na
Husna za kimahaba.
“Khaa!
Unasemaje? Mimi siamini labda kama kuna picha zao za pamoja naomba
unitumie Whatsapp nizione maana nashindwa niongee nini, sikujua kama
walienda popote Ray na Husna.”
Mwanahabari wetu alimtumia picha hizo Chuchu lakini hadi tunakwenda mitamboni, mrembo huyo hakuwa amejibu kitu chochote.
Mwanahabari wetu alimtumia picha hizo Chuchu lakini hadi tunakwenda mitamboni, mrembo huyo hakuwa amejibu kitu chochote.
Chanzo global Publishers
COMMENTS