Rapper mkongwe Joseph Haule aka Professor Jay amesema siasa haiwezi kumtenganisha na muziki, na pia amejipanga kuja na project mpya ya...
Rapper mkongwe Joseph Haule aka Professor Jay amesema siasa haiwezi kumtenganisha na muziki, na pia amejipanga kuja na project mpya ya muziki iitwayo ‘The Icon’.
Professor ameiambia Mpekuzi kuwa, hata kama akipata nafasi ya ubunge atahakikisha mashabiki wake wanapata muziki kama kawaida.
“Nitaendelea kuwatumikia mashabiki wa muziki wangu kama kawaida,
najua sasa hivi nadeni kubwa kwenye muziki, lakini hivi karibuni
nitaachia kazi mpya kwa sababu hata huku nilikoingia nimeingia kutokana
na muziki, kwahiyo hata nikiingia bungeni bado kazi nitaendelea kufanya,
najua mashabiki wangu wanategemea muziki wetu kama chakula cha ubongo
kwahiyo mimi bado nipo kwajili ya mashiki wangu,” alisema Professor.
Pia Professor Jay amejipanga kuachia project yake mpya ya muziki ‘The
I Con’ ambayo itazungumzia maisha ya muziki wake ambayo itawashirikisha
wasanii wengine.
“Hii project itamuonyesha Professor Jay alikotoka mpaka alipofikia,
kwa sababu naamini Professor Jay ni role model wa wasanii wengi na
vijana wengi wa Tanzania, pia nimekuwa mfano bora kwa wasanii wenzangu
na vijana wengi wa Tanzinia, nimesabisha vijana wengi kuingia kwenye
muziki kutokana na harakati zangu, hata vijana wengi ukiwauliza nani
amekufanya ukaingia kwenye muziki utaambiwa ni Professor Jay, especial
wanaofanya Hip Hop na vitu kama hivyo.
Pia mafanikio yangu yamewafanya
vijana wengi kuingia kwenye muziki hata wasanii wa kuimba, pia wazazi
wengi nimejaribu kuwaaminisha kwamba muziki siyo uhuni na kuamua
kuupenda, kwaiyo hizo harakati zangu zote kwa umoja wake utaziona kwenye
The Icon, ndani ya project hiyo utakuta documentary yangu, albam na
mambo mengi sana, kwahiyo hii yote inakuja ndani ya mwaka huu wadau na
mashabiki wa muziki wangu wakae mkao wa kula,” alimalizia Professor Jay.
COMMENTS