Nhlanhla Nciza. MMOJA wa wanamuziki wanaounda Kundi la Mafikizolo la nchini Afrika Kusini, Nhlanhla Nciza, ametangaza ua...
MMOJA
wa wanamuziki wanaounda Kundi la Mafikizolo la nchini Afrika Kusini,
Nhlanhla Nciza, ametangaza uamuzi wake wa kusaidia familia zilizokimbia
makazi yao kutokana na vurugu zinazoendelea nchini humo.
Vurugu zikiendelea katika Mji wa Durban, Afrika Kusini.
Ni
wiki ya pili sasa tangu Afrika Kusini ikumbwe na vurugu zinazoambatana
na mauaji zinazosababishwa na makundi ya watu wenye silaha ambayo
yanawalaumu wahamiaji wa Kiafrika kwa kuchukua kazi zao.
Nhlanhla
amelaani mauaji hayo na kupitia akaunti yake ya Instagram hivi karibuni
amewaomba mashabiki wake, marafiki na wengine wote kuungana katika
kuwasaidia wahanga wa vurugu hizo zinazoendelea.
Rais
nchi hiyo, Jacob Zuma amesitisha ziara yake ya nchini Indonesia ili
kukabiliana na vurugu hizo huku akiwatembelea watu walioathirika.
COMMENTS