Wafuasi wa upinzani wakiwasha matairi ya magari barabarani Upinzani nchini guinea jana uliandaa maandamano ya kupinga kalenda...
Wafuasi wa upinzani wakiwasha matairi ya magari barabarani
Upinzani nchini guinea jana uliandaa maandamano ya kupinga kalenda ya uchaguzi.
Upinzani unaomba uchaguzi wa serikali za mitaa ufanyike kabla ya uchaguzi wa urais, kama jinsi mikataba mbalimbali inavyoeleza.
Uchaguzi wa urais nchini humo umepangwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Katika maandamano hayo mtu mmoja aliuawa katika mji wa Labé huku wengine wengi wakijeruhiwa.
Wiki hii rais wa Guinea, Alpha Condé, alipinga uwezekano wa tarehe ya uchaguzi wa rais kubadilishwa.
Serikali ya Guinea imebainisha kwamba maandamano yaliyoandaliwa na upinzani jana yameonesha jinsi gani upinzani hauna mipango ya maendeleo kwa wananchi, kwani maandamano hayo hayakuitikiwa na watu wengi baada ya polisi kuzidisha ulinzi katika maeneo mbalimbali.
Mshauri wa rais wa nchi hiyo Rachid Ndiaye amesema kalenda ya uchaguzi haitabadilika.
Ndiaye amebainisha kwamba kalenda ya uchaguzi inawekwa na tume huru na siyo wanasiasa.
COMMENTS