Mbunge wa Wilaya ya Temeke, Abbas Zuberi Mtemvu (kushoto) na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Ngoyai Lowassa (kulia) baada ya kumaliza...
WAZIRI Mkuu
aliyejiuzulu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Ngoyai Lowassa,
ameomba serikali iunde kamati maalum kwa ajili ya kuzuia ajali za
barabarani kwa kuwaita wahusika na kujadiliana namna ambavyo Tanzania
inaweza kuepukana na vifo vitokanavyo na ajali za barabarani.
Lowassa
aliyekuwa mgeni rasmi katika matembezi ya kulaani na kupinga mauaji ya
Albino ameyasema hayo katika Viwanja vya TCC Chang’ombe leo jijini Dar
baada ya kumalizika kwa matembezi ya kulaani na kupinga mauaji ya watu
wenye ulemavu wa ngozi (Albino) yaliyoandaliwa na kikundi cha wakimbiaji
(Jogging) kinachotambulika kama Temeke Family yaliyokuwa na kauli mbiu
ya ‘MIMI ALBINO NINA HAKI YA KUISHI’ ambao wameguswa na mauaji hayo na
kuamua kuanzisha kampeni hiyo itakayokuwa endelevu kwa kila mkoa hasa
ile mikoa iliyokithiri kwa mauaji ya albino.
“Nawapongeza
Albino kwa kudai haki zao na ninawashauri msifumbie macho suala hili
lakini pia ni wajibu wa kila Mtanzania kuliona jambo hili wanalotendewa
wenzetu ni jambo baya kwa kuwa linatuharibia heshima nyumbani na
duniani pia na ni unyama, haufai kwani tunaonekana sisi ni majambazi
tunaua binadamu wenezetu.
“Ingawa
Albino waliokufa ni wachache, 75 si wachache kwa sababu ni maisha ya
binadamu lakini binadamu wengine wengi wamekufa kwenye ajali za
barabarani. Imekuwa kama ni mchezo, ni kama kuua kuku, kila siku kila
mahali ni mambo hayahaya.
“Tumesikia
TABOA leo wameunda kamati, mimi nawapongeza kwa uamuzi huo lakini
napenda kuiomba serikali iunde hiyo kamati kwa sababu inaweza kuwaita
wahusika wenyewe na wengine. Kwa pamoja tuhakikishe tatizo hili
lisiendelee. Nawaomba Watanzania tulione jambo hili la kufa binadamu
kuwa ni jambo baya na halifai kuendelea, tuchukue hatua na tuiombe
serikali ichukue hatua zaidi,” alisema Lowassa.
Matembezi
hayo yaliongozwa na Mbunge wa Wilaya ya Temeke, Mh. Abbas Zuberi
Mtemvu, Mbunge wa Kinondoni, Mh. Idd Azzan, Mbunge wa Ilala, Mh. Mussa
Azzan Zungu, Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke, Mh. Juma Mkenga na
vikundi mbalimbali vya jogging wilaya ya Temeke na kumalizika na
burudani kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Inspekta Haroun.
COMMENTS