Watu watatu wauwawa Mandera, Kenya
HomeHabariKimataifa

Watu watatu wauwawa Mandera, Kenya

Kenya imeshuhudia mashambulizi kadhaa yaliyoshukiwa kuwa ya kigaidi ikiwemo lile la Westgate Mall, September 21, 2013.  Shambulizi  ji...


Kenya imeshuhudia mashambulizi kadhaa yaliyoshukiwa kuwa ya kigaidi ikiwemo lile la Westgate Mall, September 21, 2013. 

Shambulizi  jingine linaloshukiwa kuwa la kigaidi lilitokea Ijumaa katika mji wa Mandera uliopo kaskazini mashariki mwa Kenya na kusababisha vifo vya watu watatu wakiwemo maafisa wa polisi wawili na watu saba walijeruhiwa.
Ingawa hakuna kundi lolote la kigaidi linalodai kuhusika  na shambulizi  hilo, watu hao watatu waliofariki walikuwa kwenye msafara wa gavana wa jimbo la Mandera, bwana  Ali Roba walipokuwa wakirudi kazini baada ya shughuli za kikazi.  Habari zaidi zinasema gari moja limeharibiwa kabisa kwenye shambulio hilo.


Duru za kiusalama zinasema shambulio hilo limetokea karibu sana na barabara ya Arebia ambapo abiria wasiopungua 28 waliuwawa mwezi Novemba mwaka jana ndani ya basi lililokuwa safarini kurudi mjini Nairobi kutoka mji wa Mandera.
Katika shambulio hilo la mwaka jana kundi la wanamgambo wa al-Shabab la nchini Somalia lilidai kuhusika  na tukio hilo.
Taarifa juu ya shambulizi la Ijumaa zilisema gavana Robo hakujeruhiwa kwa sababu gari lake lilikuwa limeshapita wakati tukio likitokea.
Shambulizi la mwaka jana mjini Mandera, Nov. 22, 2014.Shambulizi la mwaka jana mjini Mandera, Nov. 22, 2014.

Wakazi wa mji wa Mandera walisema mji huo umejaa wasiwasi wa mashambulizi ya aina hiyo yanayohusishwa na ugaidi ambayo huwakumba watu wa jamii zote yaani wakristo na waislam.
Kenya  imeshuhudia mashambulizi ya mara kwa mara yanayosababisha vifo yakidaiwa kufanywa na kundi la wanamgambo wa al-Shabab lenye makao yake nchini Somalia kufuatia Kenya kupeleka wanajeshi wake nchini humo ili kuisaidia serikali ya Somalia  kupambana na wanamgambo hao wanaodumaza hali ya usalama nchini humo
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Watu watatu wauwawa Mandera, Kenya
Watu watatu wauwawa Mandera, Kenya
http://gdb.voanews.com/A18A9B65-D2DE-48EA-BBEE-9C98ECBC27BC_w640_r1_s.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/03/watu-watatu-wauwawa-mandera-kenya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/03/watu-watatu-wauwawa-mandera-kenya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy