wa Geita limewakamata waganga wa kienyeji 32 wanaopiga ramli chonganishi katika msako uliofanywa hivi karibun...
wa
Geita limewakamata waganga wa kienyeji 32 wanaopiga ramli chonganishi
katika msako uliofanywa hivi karibuni ili kuhakikisha mauaji ya vikongwe
na watu wenye ulemavu wa ngozi yanakomeshwa kabisa.
Akizunguza
na waandishi wa habari baada ya kufanya msako na kuwakamata waganga hao
kamanda wa polisi mkoa wa Geita Sacp Joseph Konyo amesema waganga
hao wamekamatwa wakiwa na vifaa mbalimbali ambavyo ni matunguri na
ngozi za wanyama kama vile simba chui na nyati vikiwa vimekaushwa.
Kamanda
Konyo mesema sasa wakati umefika wa kuhakikisha mauaji yanayotokana na
imani potofu za kishirikina yanakomeshwa na ili kuyakomesha watu wa
kwanza kudhibitiwa ni waganga wa kienyeji wanaofanya shughuli zao pasipo
kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na nchi.
Kamanda
Konyo amesema upo ushahidi wa wazi unaonyesha mahusiano ya karibu ya
mauaji haya ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi na waganga wa
kienyeji kwani ndio wahusika wanaoagiza viungo vya Albino na ndio hao
wanaopiga ramli za uongo kuonyesha kuwa vikongwe hasa wanawake ndio
wachawi.
Ameongeza kuwa jeshi la Polisi haliwezi kuhangaika na watu wengine wakati huku waganga ndiyo wanaosababisha mauaji hayo ya walemavu wa ngozi na vikongwe huku wakisababisha wananchi kuacha kufanya shughuli zao za kila siku
Kamanda
Konyo amesema serikali haiwezi kuvumilia waganga wa namna hii
wanaoipotosha jamii hivyo msako huu utaendeshwa katika mikoa yote
Tanzania bara ili kubaki na jamii salama isiyokuwa na vitisho vya mauaji
ya kikatili kama haya.
Baadhi
ya wananchi mkoa wa Geita wameipongeza hatua ya serikali kuanza sasa
kuwachukulia hatua watuhumiwa wote wanaopatikana na tuhuma za mauaji
yanayotokana na mila potofu na ushirikina.
COMMENTS