Nyota wa bongo fleva Young Killer Msanii wa muziki wa ki...
Nyota wa bongo fleva Young Killer
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Young Killer, amesema ana ndoto za kufikia mafanikio aliyonayo mwanamuziki wa kimataifa, Jay Z.
Akizungumza na Mwandishi jijini Dar es Salaam, Killer, alisema dhamira yake ni kuwa msanii mkubwa kama huyo wa Marekani.
“Natamani siku moja nifikie uwezo na mafanikio kama ya Jay Z, nampenda sana,” alisema Killer.
Gwiji wa muziki wa hip hop Jay Z
“Hizo ndizo ndoto zangu za kusonga mbele zaidi, napenda kuiga anayofanya nguli huyo wa Marekani,” alisema msanii huyo.
COMMENTS