Juan Mata akishangilia goli la kwanza dhidi ya Liverpool Timu ya Manchester United imeibuka na ushindi dhidi ya watani wao jadi Liverpool....
Juan Mata akishangilia goli la kwanza dhidi ya Liverpool
Timu ya Manchester United imeibuka na ushindi dhidi ya watani wao jadi Liverpool.
Juan Mata akifunga goli la kwanza
Man United ambayo kwa sasa inashika nafasi ya nne ilipata ushindi wa 2-1 dhidi ya majogoo hao wa Liverpool katika dimba la Anfield.
Akifungwa goli la pili
Magoli yote ya Mashetani Wekundu yalifungwa na Juan Mata huku goli la kufuatia machozi la Liverpool likifungwa na mshambuliaji machachari Daniel Sturridge.
Mechi hiyo ilikuwa ya kipekee baada ya Mr Liverpool Steven Gerrard kuingia kipindi cha pili na kuchezwa sekunde kadhaa kabla hajalimwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya kiungo Ander Herrera.
Hii huenda ikawa ni mechi ya mwisho kwa Steven Gerrard dhidi ya Man United baada ya kutangaza kutangaza kuondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu.
Steven Gerrard akitoka uwanjani baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu
Juan Mata amezima ngebe za Liverpool ambao walipania kushinda mechi hii kulipiza kisasi cha mechi ya kwanza walionyukwa 3-0 Old Trafford Desemba mwaka uliopita.
COMMENTS