Mshambulizi mahiri wa Paris Saint-Germain Zlatan Ibrahimovic amewakosoa vibaya wachezaji wa Chelsea mara baada ya kumzonga mwamuzi ku...
Mshambulizi
mahiri wa Paris Saint-Germain Zlatan Ibrahimovic amewakosoa vibaya
wachezaji wa Chelsea mara baada ya kumzonga mwamuzi kupitiliza hali
iliyosababisha kupewa kadi nyekundu.
Baada ya tukio hilo kutokea Ibrahimovic amewaita wachezaji wa Chelsea kuwa ni watoto 11 ambao walikuwa wamemzunguka.
Mchezaji
huyo raia wa Sweden alitolewa nje mara baada ya kuzawaidiwa kadi
nyekundu katika dakika ya 31 baada ya kumchezea madhambi Oscar, huku
John Terry, Nemanja Matic na Gary Cahill wakimzonga punde tu baada ya
tukio hilo.
Ibrahimovic ameendelea kusema kuwa hakuridhishwa hata kidogo na tabia ambayo waliionyesha wachezaji wa Chelsea.
"Nilipoiona
ile kadi nyekundu nikahisi kama mwamuzi hajui anachokifanya kiukweli,
nilihisi pengine aliona kitu tofauti aisee," alisema Zlatan.
"Na
kibaya zaidi kilichonisikitisha ni pale nilipoona wachezaji wa Chelsea
wamenizunguka hasa baada ya kupewa ile kadi nyekundu, nilihisi kama kuna
watoto 11 hivi wamenizunguka, nikaamua kuondoka zangu kwa sababu
niliona na mwamuzi pia anakuja.
"Kiukweli
sijui kama kweli Oscar aliumia au alikuwa anaigiza, lakini haijalishi,
sio mbaya, muhimu ni kwamba tumefanikiwa kushinda mchezo huu, ngoja sasa
tuangalie nini kitatokea mbeleni huko."
COMMENTS