Alex Oxlade-Chamberlain hatokuwepo kwa mwezi mmoja Kocha wa Arsenal Arsene Wenger atalazimika kuji...
Alex Oxlade-Chamberlain hatokuwepo kwa mwezi mmoja
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger atalazimika kujikuna kichwa baada ya kupata habari kuwa kiungo chake cha kutegemewa Alex Oxlade-
Chamberlainhatakuwepo kwa takriban majuma tatu hadi nne zijazo kutokana na jeraha nyuma ya goti.
Kulingana
na kocha huyo,Chamberlain alipata jeraha hilo katika mechi ya kukata na
shoka ya FA dhidi ya wapinzani wao wa jadi Manchester United jumatatu
iliyopita.
Kujeruhiwa kwake ni pigo kwa azimio la Arsenal
kuimarisha matokeo yao katika ligi kuu ya Uingereza ambapo sasa
wanashikilia nafasi ya tatu .
Alex Oxlade-Chamberlain alichangia pakubwa katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester united katika FA
Aidha Arsenal wanajiandaa kwa
mechi ya marudio ya mkondo wa 16 bora katika ligi kuu ya mabingwa barani
Ulaya ambapo wameratibiwa kuchuana dhidi ya Monaco juma lijalo.
Winga huyo alikuwa amerejea mwishoni mwa mwezi Februari baada ya kukaa mwezi mmoja nje kufuata jeraha lengine la kiuno.
Wenger
hata hivyo alipata afueni katika safu ya ulinzi baada ya kurejea kwa
Gabriel aliyejeruhiwa katika mechi ngumu dhidi ya QPR mnamo Machi
tarehe 4.
Loaded All PostsNot found any postsVIEW ALLReadmoreReplyCancel replyDeleteByHomePAGESPOSTSView AllRECOMMENDED FOR YOULABELARCHIVESEARCHALL POSTSNot found any post match with your requestBack HomeSundayMondayTuesdayWednesdayThursdayFridaySaturdaySunMonTueWedThuFriSatJanuaryFebruaryMarchAprilMayJuneJulyAugustSeptemberOctoberNovemberDecemberJanFebMarAprMayJunJulAugSepOctNovDecjust now1 minute ago$$1$$ minutes ago1 hour ago$$1$$ hours agoYesterday$$1$$ days ago$$1$$ weeks agomore than 5 weeks agoFollowersFollowTHIS CONTENT IS PREMIUMPlease share to unlockCopy All CodeSelect All CodeAll codes were copied to your clipboardCan not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy
COMMENTS