AMA kweli binadamu siyo waoga! Watu wawili ambao majina yao hayakupatikana mara moja, waliamua kujitoa fahamu na ...
AMA kweli
binadamu siyo waoga! Watu wawili ambao majina yao hayakupatikana mara
moja, waliamua kujitoa fahamu na kuamua kufanya mapenzi ndani ya gari
nje ya Kituo cha Polisi cha Alimaua kilichopo Kata ya Kijitonyama jijini
Dar, OFM wanakumegea mkanda mzima.
Watu hao wakiendelea kufanya mambo yao.
Tukio
hilo la aina yake lilinaswa saa nane usiku wa Jumatano wakati kikosi
kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kikiwa kazini kusaka matukio
mbalimbali ya usiku mnene.
Ilikuwaje?
Ilikuwaje?
Awali,
baadhi ya watu waliokuwa wakitoka kuangalia mechi ya Kombe la Capital
One kati ya Chelsea na Liverpool nchini Uingereza waliwaona wawili hao
wakipaki gari eneo hilo la polisi kana kwamba walikuwa na shida muhimu
ya kiusalama kama si kisheria. Kituo hicho kilikuwa kimefungwa!
Tofauti
na matarajio ya mashuhuda hao, gari hilo aina ya Toyota Mark II (namba
za usajili tunazo) lilizimwa taa za ndani na kuachwa ikiunguruma kisha
watu hao ambao haikufahamika kama ni wapenzi au ni changudoa na mteja
wake walianza kushikana kimahaba.
DEREVA ALALIA USUKANI
OFM
walizidi kuambiwa kuwa, mashuhuda walijiongeza na kubaini kwamba wawili
hao walikodi gari hilo kwani walipoanza kushikana, dereva aliegemea
usukani kwa hali iliyotafsirika kuwa, alikuwa akiwapa nafasi abiria wake
wamalize ‘mambo’ yao.
He! Mchezo wAnoga
He! Mchezo wAnoga
“Unaweza
kusema wawili hao walikuwa ndani ya fensi nyumbani kwao, kwani wanazidi
kufanyiana mambo ya chumbani. Hivi hapa sisi tunawashangaa,” shuhuda
mmoja aliwaambia OFM.
OFM WATINGA
Ndani
ya dakika chache, makamanda wa OFM wanaopatikana kwa saa 24, walikuwa
wamewasili eneo la tukio kwa kutumia pikipiki zao maalum ziendazo kasi.
Kitendo bila kuchelewa, zoezi la kuwafotoa picha kwa mbali lilianza na ndipo waliposhituliwa na mwanga wa ‘flash’, hali iliyomfanya dereva wa gari hilo kutaka kuondoa gari.
Kitendo bila kuchelewa, zoezi la kuwafotoa picha kwa mbali lilianza na ndipo waliposhituliwa na mwanga wa ‘flash’, hali iliyomfanya dereva wa gari hilo kutaka kuondoa gari.
WATAITIWA, WAKUTWA CHAKARI
Kwa kutumia ujasiri wa hali ya juu, makamanda hao kwa kusaidiana na mmoja wa mashuhuda anayeishi eneo hilo walilizuia gari lisiondoke na ndipo ilipobainika kuwa, licha ya kunaswa wakiibanjua amri ya sita ya Muumba pia watu hao walikuwa chakari kwa pombe.

WASHINDWA KUJIBU MASWALI
Hata hivyo, kutokana na kuwa tilalila, ilikuwa vigumu kuwahoji kwani kila walipoulizwa kwa nini waliamua ‘kupumzikia’ nje ya kituo hicho cha polisi, waliishia kuinamisha vichwa.
Hata hivyo, kutokana na kuwa tilalila, ilikuwa vigumu kuwahoji kwani kila walipoulizwa kwa nini waliamua ‘kupumzikia’ nje ya kituo hicho cha polisi, waliishia kuinamisha vichwa.
OFM YAMTOA NDUKI DEREVA
Mazingira hayo yaliwalazimu makamanda wa OFM kumwamuru dereva ambaye alikuwa akijitambua kuliondoa gari hilo kituoni hapo kabla msala mkubwa haujawapata.
Zote hizo pombe
Mazingira hayo yaliwalazimu makamanda wa OFM kumwamuru dereva ambaye alikuwa akijitambua kuliondoa gari hilo kituoni hapo kabla msala mkubwa haujawapata.
Zote hizo pombe
Uchunguzi
uliofanywa na OFM umebaini kuwa, kitendo cha watu hao kupaki gari eneo
la kituo cha polisi na kufanya uzinzi kilitokana na pombe walizokuwa
wamekunywa hivyo akili yao iliwatuma kuwa lile lilikuwa eneo salama
zaidi kwao.
OFM WAMSAKA KAMANDA WA POLISI
Ili kutaka kujua ni kwa nini kituo hicho cha polisi kilipigwa ‘loki’ wakati usiku ndiyo matukio ya uhalifu yako kwa wingi, OFM walimwendea hewani Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura.
OFM: “Afande, habari?”
Wambura: “Nzuri.”

OFM: “Naongea na RPC wa Kinondoni?”
Wambura: “Unasemaje?”
Wambura: “Unasemaje?”
OFM: “Mimi ni mwandishi napiga simu kutoka Global Publishers...”
Wambura: “Nipo kwenye mkutano. Nenda ofisini (Oysterbay Polisi) utamkuta mhusika.”
OFM: “Naomba unisaidie pale nitamkuta nani? Au namba yake ya simu.”
Wambura: “Nipo kwenye mkutano. Nenda ofisini (Oysterbay Polisi) utamkuta mhusika.”
OFM: “Naomba unisaidie pale nitamkuta nani? Au namba yake ya simu.”
Wambura:
“Ifike mahali sasa, waandishi muwe mnafika ofisini kwa taarifa kama
hizi (za kiofisi). Nitajuaje kama wewe ni mwandishi? Nenda pale
utaoneshwa kaimu kamanda uzungumze naye.”
OFM OYSTERBAY POLISI
OFM walifunga safari hadi Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar na kumuulizia kaimu kamanda wa mkoa lakini afande aliyekuwa mapokezi alisema ametoka kikazi nje ya kituo.
OFM OYSTERBAY POLISI
OFM walifunga safari hadi Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar na kumuulizia kaimu kamanda wa mkoa lakini afande aliyekuwa mapokezi alisema ametoka kikazi nje ya kituo.
COMMENTS