SAKATA la wasichana wawili warembo, Maua Sadick (24) mkazi wa Stakishari, Ukonga, Dar es Salaam na Lucy Fred ...
SAKATA la
wasichana wawili warembo, Maua Sadick (24) mkazi wa Stakishari, Ukonga,
Dar es Salaam na Lucy Fred (23) mkazi wa Karakata, Dar ambao
walishikiliwa katika Kituo cha Polisi Stakishari, Ukonga jijini kwa
madai ya kufanya mapenzi ya jinsia moja limechukua sura mpya.
Habari
za kipolisi zinasema wasichana hao ambao walifunguliwa jalada kituoni
hapo namba SKT/RB/463/2015 baada ya kukamatwa Januari 12, mwaka huu
inadaiwa kuwa walioana.
“Zipo
picha zinazodaiwa kuwa walioana na wanaonekana wakiwa wanavishana pete
nyingine wakiwa wanafungua shampeni kwenye hafla fupi ambayo waliifanya
jijini Dar es Salaam,” kilisema chanzo ndani ya jeshi la polisi.
Habari
zaidi zinadai kuwa hafla hiyo waliifanyia katika ukumbi mmoja (jina
tunalihifadhi) ambao upo Chang’ombe na unatumika kwa shughuli nyingi za
burudani na hata michezo.“Mimi nilihudhuria sherehe hiyo na picha ninazo
ambazo zinawaonesha wasichana hao wakivishana pete na walikuwepo pia
waalikwa kama unavyoona kwenye sherehe za harusi katika jamii yetu,”
alisema mtu mmoja ambaye jina lake tunalihifadhi.
Mtu
huyo alidai kuwa mmoja wa wasichana hao anamfahamu kwa kuwa sasa hivi
anaishi kwa dada yake karibu na Uwanja wa Ndege, Karakata nyuma ya
msikiti mpya.Mara baada ya kukamatwa wasichana hao, Mwenyekiti wa
Serikali ya Mtaa wa Mogo, Stakishari,George Mtambalike alilithibitishia
gazeti hili ofisini kwake kutiwa mbaroni kwao kwa madai ya kufanya
mapenzi ya jinsia moja.
Naye
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Mary Nzuki alisema
wasichana hao bado wanapelelezwa. “Ni kwamba kesi yao ipo Stakishari na
uchunguzi dhidi yao ukikamilika watafikishwa mahakamani, “ alisema
Kamanda Nzuki.
COMMENTS