WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) wameshukuru kulipwa mish...
Hata hivyo siku saba hizo zitaanza kuhesabiwa baada ya tarehe 26,
mwezi huu, ambapo pamoja na hilo, pia wameazimia mambo mengine mawili
ikiwemo kutaka kukutana na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe.
Akizungumza na gazeti hili, Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi
wa Reli nchini (Trawu) Kanda ya Dar es Salaam, Yassin Mleke alisema,
wamekubaliana kupokea mishahara hiyo ya miezi minne huku wakitaka
mishahara iliyobaki ilipwe haraka iwezekanavyo.
Alisema wameazimia kutoa siku saba baada ya tarehe 26 kwa mamlaka
hiyo kuwalipa mishahara ya mwezi Desemba mwaka jana na Januari, mwaka
huu na wasipokamilisha, watawaburuza mahakamani.
“Tumeazimia hayo matatu lakini jambo kubwa ni kwamba tunahitaji
uongozi uliopo madarakani uondoke kwa sababu umeshindwa kazi, Waziri aje
tuongee nae tujadili hatma ya Tazara, matatizo haya yaishe,” alisema
Mleke.
Jana Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), TRAWU na
wafanyakazi hao, walikutana na kufikia maazimio hayo ambayo alipewa
Naibu Katibu Mkuu wa TRAWU, Hezron Kaaya kwa ajili ya kuyafikisha
panapostahili.
Tayari menejimenti ya mamlaka hiyo imewalipa wafanyakazi hao
mishahara ya miezi minne na kubaki wa mwezi mmoja ambao wanafanyakazi
hao wanataka walipwe haraka iwezekanavyo.
Wafanyakazi hao 1,500 waliitisha mgomo kutokana na kutolipwa
mishahara yao ambapo mgomo huo uliathiri shughuli za usafiri kwa abiria,
kabla ya Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi kuubatilisha mgomo huo.
COMMENTS