Muigizaji wa filamu hapa bongo na Mwanamitindo Jokate Mwegelo na Elizabeth Michael ‘Lulu”. hivi karibuni walishindanishwa kwa urembo na ...
Muigizaji wa filamu hapa bongo na Mwanamitindo Jokate Mwegelo na
Elizabeth Michael ‘Lulu”. hivi karibuni walishindanishwa kwa urembo na
muonekano katika picha zinazoonekana mitandaoni nchini na Jokate
Mwegelo kuibuka msindi kwa kumshinda mshindani wake ,Elizabeth Michael
‘Lulu”.
Mtandao mmoja wa hapa nchini umeendesha zoezi la kuweka picha zao
kali zinazowaonesha wote wawili wakiwa na muonekano na picha kali huku
wakiuliza nani zaidi ya mwenzake.Jokate ameibuka mshindi kwa kupigiwa
kura tano huku watu wakimsifia kuwa ni wa kimataifa zaidi ambapo Lulu
alionekana kupigiwa kura na mtu mmoja.
Akizungumzia ushindi huo Jokate aliwashukuru Watanzania kwa
kumpenda na kumpa nafasi lakini aliwasihi kwa kuwaambia kuwa yeye
aonavyo wote ni warembo.“Mimi naona sisi wote ni warembo, nawashukuru
Watanzania walionichagua na kuniona nafaa,” alisema Jokate
Source: GPL
COMMENTS