Mwanamfalme Andrew Kasri ya Buckingham imepinga madai kwamba mmoja ya wana wa malkia Elizabeth mwanamfalme Andrew amekuwa alijihusi...
Mwanamfalme Andrew
Kasri ya Buckingham imepinga madai
kwamba mmoja ya wana wa malkia Elizabeth mwanamfalme Andrew amekuwa
alijihusisha katika tabia mbaya baada ya kubainika kwa nakala za
mahakamani nchini Marekani zinazomuhusisha na madai ya unyanyasaji wa
kijinsia.
Taarifa ya kasri hiyo imeelezea madai hayo kwamba mwanamfalme huyo alifanya tendo la ngono na msichana mdogo kama yasio kuwa ya kweli.
Tuhuma hizo zimetolewa katika kesi inayomuhusisha rafiki moja wa zamani wa mwanamfalme Andrew, tajiri Jefferey Epstein ambaye ameshtakiwa kwa visa vya unyanyasaji wa kijinsia.
Katika nakala zilizopatikana katika mahakama ya huko Florida,mwanamke mmoja anadai kwamba alilazimishwa na Epstein kufanya tendo la ngono na watu wengine akiwemo mwanamfalme huyo wakati msichana huyo alipokuwa na miaka 17,ambao ni umri mdogo wa kuweza kuruhusu tendo kama hilo nchini Marekani.
COMMENTS