EU yazindua miradi ya kupambana na ugaidi duniani
Katibu mkuu wa Arab League, Nabil Al-Araby (L) akipeana mkono na mkuu wa masuala ya nje wa EU,Federica Mogherini huko Brussels, Jan. 19, 2015
HomeHabariKimataifa

EU yazindua miradi ya kupambana na ugaidi duniani

Katibu mkuu wa Arab League, Nabil Al-Araby (L) akipeana mkono na mkuu wa masuala ya nje wa EU,Federica Mogherini huko Brussels, Jan. 1...

.
 

 
Umoja wa Ulaya-EU unazindua miradi mipya ya kupambana na ugaidi na nchi za ki-Islam na inaongeza ushirikiano wake wa kijasusi baada ya mashambulizi yaliyosababisha vifo nchini Ufaransa na mapambano ya ghasia huko Ubelgiji.

Mawaziri wa mambo ya nje wa EU walikutana jumatatu mjini Brussels na katibu mkuu wa Arab League, Nabil Elaraby. Baada ya hapo mkuu wa masuala ya mambo ya nje wa EU, Federica Mogherini alisema EU itashirikiana taarifa juu ya washukiwa magaidi na uwezekano wa mashambulizi na nchi nyingi kote katika dunia ya kiarabu, Afrika na Asia.

“Tulichukua uamuzi ndani ya baraza la mambo ya nje kuratibu katika njia nyingi zaidi  kuliko ilivyokuwa hadi hivi sasa. Kwanza kabisa, kwa jitihada za kushirikiana taarifa, taarifa za kijasusi, sio tu ndani ya Umoja wa Ulaya lakini pia na nchi nyingine zinazotuzunguka, kuanzia kutoka  Mediterranean na dunia ya kiarabu, kuanzia kutoka Uturuki, Misri, nchi za ghuba, Afrika kaskazini, lakini pia tukiangalia  zaidi Afrika na Asia kwa wakati fulani fulani”.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Philip Hammond
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Philip Hammond
Wakati huo huo waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Philip Hammond alisema ulaya ina azma ya kufanya kilicho  muhimu ili kuendelea kuliweka salama bara hilo. Alisema maafisa wanaangalia njia bora za kufuatilia harakati za uwezekano wa magaidi ikiwemo kushirikiana orodha za abiria wanaosafiri kwa ndege.

Kwa upande mwingine mawaziri wa EU walisema watakata rufaa  kwa uamuzi wa mahakama moja mwezi uliopita ambao uliliondoa kundi la ki-Islam la wapalestina la Hamas  kutoka kwenye orodha ya kigaidi ya EU. Hamas ilihusika katika vita vikali  vya  siku 50 na Israel mwezi Julai na Agosti mwaka jana.

Sehemu kubwa ya ulaya bado ina wasi wasi na iko kwenye tahadhari ya juu wakati waziri wa sheria wa Ubelgiji aliposema mshukiwa aliyepanga shambulizi la ugaidi lililoshindikana la wiki iliyopita bado anatafutwa.>>>>VOA
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: EU yazindua miradi ya kupambana na ugaidi duniani
EU yazindua miradi ya kupambana na ugaidi duniani
http://gdb.voanews.com/C3D7DB65-0F44-4DAB-8ADD-20BB1BF46441_w640_r1_s.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/eu-yazindua-miradi-ya-kupambana-na.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/eu-yazindua-miradi-ya-kupambana-na.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy