Emirates kumwaga ajira kwa Watanzania
Simba Yahya
HomeHabariKitaifa

Emirates kumwaga ajira kwa Watanzania

  Simba Yahya KATIKA kutekeleza moja ya malengo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiri...

KATIKA kutekeleza moja ya malengo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa hususan kuwatafutia ajira Watanzania nje ya nchi, Wizara hiyo kupitia Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu umefanikisha kulishawishi Shirika la Ndege la Emirates kuajiri Watanzania wengi zaidi kuanzia mwaka 2015.

Emirates, moja ya mashirika ya ndege tajiri zaidi duniani, linamiliki zaidi ya ndege za kisasa 280, huku likiwa na safari za uhakika duniani kote.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Simba Yahya alisema shirika hilo litaajiri Watanzania katika kada mbalimbali.

“Wamekubali kuajiri Watanzania katika kada mbalimbali, ambapo maofisa wake wanaosimamia ajira watakuja nchini (Tanzania) Machi 2015 kwa ajili ya kuwafanyia usaili Watanzania watakaoomba kazi hizo na kupata uteuzi wa awali,” alisema.

Aliwataka Watanzania kuchangamkia ajira hizo, ambazo awali zilitangazwa Julai 2014, lakini ni Watanzania wachache tu walioomba na hivyo kutofikia lengo lililokusudiwa.

“Baada ya mazungumzo ya kina, uongozi wa Emirates umekubali kuongeza muda wa kuzitangaza ajira hizo kwa mara nyingine na kupanga kufanya usaili kama ilivyoelekezwa hapo awali,” alisema.

Aliwasisitiza Watanzania wenye sifa na vigezo stahiki, kutumia fursa hiyo kuomba nafasi hizo na pia kujiandaa vyema katika usaili ili wajihakikishe ajira katika soko la ajira la kimataifa.

Kaimu Mtendaji Mkuu kutoka Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA), Boniface Chandaruba aliwataka waombaji wote kuhakikisha wanapata barua kutoka wakala huo.

Chanzo Habarileo
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Emirates kumwaga ajira kwa Watanzania
Emirates kumwaga ajira kwa Watanzania
http://www.habarileo.co.tz/images/resized/images/simba-yahya_300_172.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/emirates-kumwaga-ajira-kwa-watanzania.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/emirates-kumwaga-ajira-kwa-watanzania.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy