Msanii wa Bongo Movies, Stani Bakora na binti huyo wakiwa kwenye mahaba mazito. HII kweli ni aibu funga mwaka! Msanii wa Bongo...
Msanii wa Bongo Movies, Stani Bakora na binti huyo wakiwa kwenye mahaba mazito.
HII kweli ni aibu funga mwaka! Msanii wa Bongo Movies, Stani Bakora amenaswa na paparazi wetu akivunja amri ya sita ndani ya gari na dada mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja, Amani linakupa mchapo kamili.Tukio hilo la kinyaa lilitokea hivi karibuni maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam, karibu kabisa na maegesho ya magari yanayotumiwa na ukumbi wa burudani wa New Maisha.Chanzo makini kilichomuona msanii huyo, kilimtonya paparazi wetu siku hiyo baada ya kubaini msanii huyo amekuwa na kamchezo hako kachafu kila anapokwenda klabu hapo.
Baada ya kukurupushwa.
“Huyu jamaa amekuwa na haka kamchezo ka kwenda kumalizia kwenye parking za magari sasa leo kaja na kabinti f’lani hivi, njooni mmnase,” kilisema chanzo hicho.Bila kupoteza muda, paparazi wetu alitumia usafiri wa bodaboda ndani ya dakika sifuri alifika eneo la tukio ambapo siku hiyo kwenye ukumbi wa New Maisha Club kulikuwa kuna shoo ya Bunyerobunyero iliyokuwa na watu wachache.
Mrembo huyo akiwa amejiinamia kwa aibu.
Stan na mrembo huyo baada ya kushtuka na kuona mwanga wa kamera ukiwawakia kama taa za gari, walikurupuka na kuanza kumpiga mkwara paparazi wetu ambaye alisimamia kazi yake kikamilifu ndipo mrembo huyo aliyekuwa ametinga kigauni kifupi cheusi alipotimua mbio baadaye Stan naye akamfuata na kutokomea.
COMMENTS