Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amelaumu watu fulani ndani ya chama tawala cha ZANU-PF kwamba wanapanga kumng'atua mamlakani. Aki...
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amelaumu watu fulani ndani ya chama tawala cha ZANU-PF kwamba wanapanga kumng'atua mamlakani.
Akihutubia kongamano la chama hicho, Mugabe amesema kuwa kuna majaribio ya kuwahonga wajumbe kumpinga kama kiongozi, lakini wajumbe hawawezi kupokea hongo.
Kwa hilo amesema kuwa atapambana na rushwa ndani ya chamana kukabiliana na maafisa wa chama ambao kazi yao ni kutoa hongo.
Hasira ya Mugabe iliokana na madai ya njama ya kumuua yaliyotolewa dhidi ya naibu wake Joyce Mujuru. Hata hivyo Mujuru alikanusha madai hayo ambayo yamekuwa yakimuandamana.
Mugabe alisema kutokuwepo kwa Bi Mujuru kwenye mkutano huo wa chama kunaonyesha kuwa anaogopa.
Kadhalika Mugabe amesema Mujuru ni mwizi anayepanga kumuondoa mamlakani kwa kushirikiana na maafisa wengine wa chama.
Vilveile kiongozi huyo ametupilia mbali dhana ya kujiuzulu akisema ni upuzi .
Hivi karibuni afisa mwingine mkuu wa chama tawala, Robert Gumbo aliambia BBC kwamba Mugabe amwenye umri wa miaka 90 amegeuza chama tawala na kukifanya mali yake binafsi.
COMMENTS