Palikuwa na kituko cha mwaka kilichotukia katika kituo cha polisi bulenga, wakati mwanamke mmoja alipokuwa akiomba poo na huku akimtaka ...
Palikuwa na kituko cha mwaka
kilichotukia katika kituo cha polisi
bulenga, wakati mwanamke mmoja
alipokuwa akiomba poo na huku
kumwachilia aende zake kutokana
na mumewe kuwa na hamu ya
kufanya ngono isiyo na koma.
Ruth Nakyeyune,alikuwa akilia na
hanyamazishwi kwa madhila apatayo
kutoka kwa mumewe huku akimuomba
mumewe mwenye asili ya Nigeria
bwana Sultan Ali Baba kwa pamoja
ni wakaazi wa Nakuwade
Bulenga,karibu na barabara ya
Mityana, mwanamke anaomba poo
na mwenyekusema basi yatosha na
kutaka waachane kila mmoja ashike
hamsini zake.
Bi Nakyeyune amesema pia kwamba
amekuwa si mvumilivu kwa muda
mrefu na asiyejali chochote na
hataki kusikia jibu la hapana
linapokuja suala la ngono.bibi huyo
amesema kwamba pindi anapokuwa
hajisikii vizuri na hawezi kufanya
ngono,Sultan haelewi juu ya suala
hilo,na humnunia.sultani alipoulizwa
juu ya kununa kwake alisema
kwamba hamuamini mkewe na
sababu anazompa hivyo anadai
anamdanganya na kumnyima haki
yake bure na kusema kuwa huwa
hamridhishi,mara zote mwanamke
huyoa amekuwa akitafuta sababu na
mara moja ameshawahi kumtishia
atajiua.
Sultan alimtaka mwanamke huyo
amshukuru Muumba wake kwakuwa
yeye ni mume mwema asiyekunywa
pombe kama wengine wafanyavyo,na
kumshangaa mkewe anashindwaje
kumridhisha kirahisi?
Na kumuuliza mkewe bi Nyakyeyune
kwanini aliwaacha wazazi na jamaa
zake kama hakuwa tayari
kumridhisha kingono,na kama
shangazi zake ndo walomfunda na
kumpeleka kwake kwa shughuli za
ndoa, vipi hayuko tayari?
Inaelezwa kuwa wake wa awali wa
bwana Sultan walimkimbia
mwanamume huyo kwa tabia hiyo hiyo
ya kutoridhika kingono,lakini
baadaye Sultani alimuomba mkewe
kusalia nyumbani kwa ajili ya watoto
wao ili wawalee lakini mke alikataa
ushawishi huo.
COMMENTS