Dar es Salaam. jumbe wa Klabu Arsenal ya England unatarajiwa nchini Jumapili pamoja na mengine ya soka, klabu hiyo kuwekeza nchini. ...
Dar es Salaam. jumbe wa Klabu Arsenal ya England unatarajiwa nchini Jumapili pamoja na mengine ya soka, klabu hiyo kuwekeza nchini.
Ofisa Biashara Mkuu wa Arsenal, Venkatesham
alisema jana wameichagua Tanzania kwa wana mashabiki wengi na kwa
kushirikiana na taasisi za Tanzania, watakuwa karibu zaidi na mashabiki
wao kuliko ilivyokuwa awali.
“Katika bara lenye nchi zaidi ya 50, tumechagua kuzuru Tanzania kimkakati kwa sababu tunaiamini nchi hii. Arsenal ina mamilioni ya Watanzania ambao ni mashabiki waaminifu na wenye mapenzi makubwa nayo.” Alisema katika ziara yao hiyo ya wiki moja nchini Tanzania, pia watajadili fursa za ushirikiano na wafanyabiashara kadhaa wakubwa nchini Tanzania katika soka.
Huu utakuwa ujumbe wa kwanza wa Arsenal kutua Tanzania, ambao klabu hii kubwa ya Uingereza inataka kujenga ushirika mkubwa katika maeneo ya masoko na chapa zake, ili kutanua mafanikio yaliyofikiwa kwenye nchi nyingine za Afrika kama Kenya, Uganda na Nigeria.
Washika Bunduki hao wa London wanataka kutoa fursa kwa benki za Tanzania pamoja na kampuni za simu na taasisi nyingine kupata rasilimali zihusianazo na Arsenal, kama vile bidhaa zilizosainiwa kwa majina ya wachezaji, tiketi za mechi.
Chanzo Mwananchi
COMMENTS