VIJANA WATATU WALIOTAKA KWENDA IKULU WAISHIA RUMANDE DAR!

VIJANA watatu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, wamekamatwa na polisi eneo la Magomen...


VIJANA watatu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, wamekamatwa na polisi eneo la Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 2, 2014, baada ya jaribio lao la kufanya matembezi kutoka mkoa wa Geita wakielekea Ikulu ya Dar es Salaam kumuona Rais Jakaya Kikwete kufikisha malalamiko yao.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana, vijana hao watatu, Juma Maganga, Khalifa Selemani na Athanas Michael, walielekezwa na maafisa usalama kumuona yeye DC baada ya kuwasili kwenye eneo lake la utawala wakitokea Geita, ili awape baraka za kwenda Ikulu. Lakini walipofika ofisini hapo, DC huyo alitaka kujua nini hasa kilichowafanya watembee safari ndefu kama hiyo?
         DC Rugimbana alisema, walimweleza kuwa Mosi, Wanataka Kumnuona Rais ili wamueleze kuchukizwa kwao na vitendo vya viongozi kula rushwa na hakuna hatua dhabiti zinazochukuliwa dhidi yao, kukithiri kw amatumizi mabaya ya rasilimali za taifa, kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji dhidi ya raia, na kudai kurejeshwa kwa serikali ya Tanganyika.
Baada ya kusikia hayo, DC aliwaeleza kuwa kila Mtanzania anayo haki ya kumuona Rais wa nchi, hata hivyo sio kumuona kiholela bali ni kwa utaratibu maalum, na kwa kufikia hatua waliyofikia vijana hao, tayari walikuwa wamevunja sheria lakini akawataka wasubiri awasiliane na wakubwa ili waandaliwe utaratibu wa kumuona Rais.

Hata hivyo vijana hao walikataa na walipotoka nje ya ofisi ya DC hapo Kinondoni, walifanya tena jaribio la kuelekea Ikulu na safari hii polisi hawakufanya masihara, waliwaweka chini ya ulinzi mita chache kutoka taa za kuongozea magari kwenye makutano ya barabara za Morogoro na Kawawa ukiwa uneelekea Kariakoo. 
Vijana hao wakiwa kwenye safari yao eneo la Magomeni Kagera 
Vijana hao wakiwa chini ya ulinzi wa polisi wakielekea kituo cha polisi Magomeni Mapipa 
Polisi wa kutuliza ghasia akiwahi sehemu walikoelekea vijana hao tayari kuwakamata 
Polisi wakionye raia kutounga "tela" safari ya vijana hao wakati wakiwa eleo la Magomeni Mwembechai 
Polisi wakimdhibiti mmoja w avijana wasiokubali "kupitwa" 
Polisi wakiwahi kukamata vijana 
Vijana wakiwa chini ya ulinzi 
Wakionyesha mshikamani baada ya kukamatwa 
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana, akiwaeleza waandishi wa habari matokeo ya mazungumzo yake na vijana hao.

COMMENTS

BLOGGER
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,2861,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: VIJANA WATATU WALIOTAKA KWENDA IKULU WAISHIA RUMANDE DAR!
VIJANA WATATU WALIOTAKA KWENDA IKULU WAISHIA RUMANDE DAR!
http://4.bp.blogspot.com/-ekY9SrrhNKI/VKbbaWe0O2I/AAAAAAAA1YQ/2Vzmyj2QBaI/s640/SRRRRRR.JPG
http://4.bp.blogspot.com/-ekY9SrrhNKI/VKbbaWe0O2I/AAAAAAAA1YQ/2Vzmyj2QBaI/s72-c/SRRRRRR.JPG
Antagon Blog
http://antagonf.blogspot.com/2015/01/vijana-watatu-waliotaka-kwenda-ikulu.html
http://antagonf.blogspot.com/
http://antagonf.blogspot.com/
http://antagonf.blogspot.com/2015/01/vijana-watatu-waliotaka-kwenda-ikulu.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy