Fasihi simulizi na Chimbuko la Riwaya

Fasihi simulizi na Andishi HISTORIA YA FASIHI SIMULIZI YA KIAFRIKA KWA MTAZAMO WA NADHARI ZA UTANDAWAZI, UTAI...


Fasihi simulizi na Andishi

HISTORIA YA FASIHI SIMULIZI YA KIAFRIKA KWA MTAZAMO WA NADHARI ZA UTANDAWAZI, UTAIFA NA HULUTISHI.
 
Utangulizi
Fasihi simulizi kwa mujibu wa Mlokozi (1996), ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya mdomo na vitendo bila kutumia maandishi. Hivyo fasihi simulizi inafungamana na muktadha au mazingira fulani ya kijamii na kutawaliwa na muingiliano wa mambo kama vile Fanani, Hadhira, Fani inayotendwa, Tukio, Mahali pamoja na Wakati wa utendaji.


Balisidya (1983) anasema fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa, kuwasilishwa na kusambazwa kwa wasikilizaji na watumiaji wake.


Mteru,M (1983) anasema fasihi simulizi ni aina ya fasihi inayotumia mdomo kwa kuumba na kusambaza.


Fasili zote zinazungumzia kitu kilelekile kwamba fasihi simulizi inategemea sana uwepo fanani, hadhira, jukwaa na mada inayotendwa. Hivyo kwa ujumla tunaweza kusema kuwa Fasihi simulizi ni sanaa inayotumia lugha ya kisanaa ili kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa kwa njia ya mdomo au masimulizi.


Kwa upande wa nadharia, tunaweza kusema kuwa nadharia, ni mawazo au muongozo unaomuongoza mtafiti au mchambuzi wa jambo Fulani ili kuweza kulikabili jambo hilo ambalo halijapata kupatiwa ufumbuzi au ukweli wake.


Nadharia ya fasihi simulizi ilianza katika elimu ya ushairi wa Wagiriki toka karne ya 18. Mnamo karne ya 20 nadharia za fasihi simulizi zimezua mikabala mikubwa katika usomaji wa matini. Kwa hiyo nadharia ya fasihi simulizi ni mawazo yanayotoa muongozo kuhusu muelekeo wa jambo Fulani katika fasihi simulizi. Kwa kufanya hivyo nadharia hizo zimeweza kuleta mabadiliko katika nadharia asilia zilizokuwepo kwa mfano utamaduni wetu wa asili kama vile ususi, ufinyanzi, jando na unyago umeathiriwa na ujio wageni.


MJADALA Watafiti wa kimagharibi na wa kiafrika wameangalia mambo mengi yaliyoikabili fasihi simulizi ya kiafrika na mawazo yao ni kama yafuatavo:

Kwa kuanza na mawazo ya wana nadharia ya utandawazi na ambayo imegawanyika katika makundi matatu ambayo ni:


Nadharia ya Ubadilikaji taratibu. Muasisi wa nadharia hii ni Charles Dawin (1809-1882), na wafuasi wake waliamini kuwa kuna misingi anuai kuhusu kanuni zinazoongoza asili na maendeleo ya utamaduni wa mwanadamu. Kundi hili liliona kuwa dhana ya ubadilikaji taratibu misingi yake mikuu ni Viumbe hai.


Wanasema Viumbe hai vyote vinakuwa katika mchakato wa mabadiliko mbalimbali hadi kufikia kwenye maumbo yao ya sasa. Hivyo na Fasihi simulizi imepitia michakato mingi ya mabadiliko mpaka kufikia katika umbo lake la sasa mfano Fasihi simulizi ya kipindi cha Ujima ni tofauti na fasihi iliyofuata katika vipindi vingine kama vile wakati wa Utumwa, Ubepari hata mfumo tulionao sasa.


Hivyo fasihi similizi ya kiafrika hubadilika kutoka kipindi kimoja hata kingine kutokana na mabadiliko ya kijamii. Kwa ujumla wasisi hawa wanaamini kuwa chimbuko la fasihi simulizi ni jamii yenyewe na kutokea kwa kufanana kwa kazi za fasihi simulizi kutoka jamii moja hadi nyingine kunasababishwa na hatua sawa za mabadiliko kiakili na kijamii kwani jamii moja iliyozagaa ulimwenguni kote akili zao ni sawa.


Nadharia ya Msambao, Waasisi wa nadharia hii ni Grimms na Thompson. Wanamsambao wamepingana na wanaubadilikaji taratibu ambao (wanaubadilikaji taratibu) waliamini kuwa kufanana kwa fani mbili za kifasihi kunatokana na jamii hizo kupitia hatua sawa za kimaendeleo, wanamsambao wanaamini kuwa pale ambapo kufanana kwa namna hiyo kutatokea sababu ya msingi ya mfanano huo ni kuwa katika kipindi fulani hapo zamani jamii hizo ziliwahi kukutana kwa namna fulani na makutano hayo yalisababisha hali ya kuazimana baadhi ya mila na desturi.


Kwa ujumla mawazo ya wafuasi wa nadharia hii wanaamini kuwa utamaduni unaweza kusambaa kutoka katika jamii imara na maarufu tena yenye nguvu kuelekea katika utamaduni wa jamii iliyo dhaifu. Hivyo basi kutokana na mawazo ya wataalamu hawa ni kuwa fasihi simulizi ya kiafrika ilisambaa kutoka katika sehemu moja iliyostaarabika (Ulaya) kwenda sehemu nyingine ambayo haijastaarabika (Afrika). Kwa mfano ushairi wa simulizi wa kiswahli ulitoka Uarabuni na uajemi kuja Afrika na huko ndiko ambako kulionekana kuwa kumesataarabika kuliko Afrika na ndio maana ushairi huo uliletwa huku Afrika.


Wananadharia hii wanaamini kuwa asili ya fasihi simulizi ya kiafrika ni ulaya, jambo ambalo hatuwezi kukubaliana nalo kwani kila jamii ina fasihi yake na kutokea mfanano wa baadhi ya kazi za fasihi huenda kuna kuathiriana kwa namna Fulani miongoni mwa jamii hizo.


Nadharia ya Kisosholojia. Nadharia hii ya kisosholojia ina mihimili mitatu ambayo ni ule wa Umahususi na sio umajumui, mkazo katika utendaji na mhimili unaosisitiza dhima ya fasihi simulizi katika jamii.


Kwa kuanza na mhimili wa Umahususi, nadharia hii ilijikita zaidi katika jamii peke yake badala ya kujikita katika taaluma ya sanaa jadi kwa ujumla kama walivyofanya wananadharia wa nadharia ya kiutandawazi. Hii ilikuwa baada ya kugundua dosari zilizofanywa hapo kabla, Dosari ya kutoa tamko la juu juu na la jumla zaidi ambapo matamko hayo mara nyingi yalitupilia mbali vipengele fulani vya lugha na mienendo mingine ya jamii.


Pia katika mhimili wa utendaji, Wanasosholijia waliweka msisitizo katika kuchunguza utendaji (performance) wa kazi mbalimbali ya fasihi simulizi. Kutokana na msisitizo huo imebainika kuwa fanani wa kazi ya fasihi wanaujuzi na ustadi wa kiutendaji katika sanaa husika na jambo hili limetuwezesha kuelewa kuwa katika fasihi simulizi kuna kipengele cha utendaji. Vilevile wamedokeza sifa za ndani za fasihi simulizi ya kiafrika, na hivyo wao wanaona kuwa ili kujua fasihi simulizi ya kiafrika ni vyema kuangalia jamii na utendaji wa kazi husika.


Katika msisitizo juu ya dhima ya Fasihi simulizi katika jamii, Wanasosholijia wanaamini kuwa uamilifu wa fasihi simulizi upo hai na haufi na kwamba unabadilika kulingana na maendeleo ya jamii husika.


Hivyo ili kuelewa historia ya fasihi simulizi kutokana na mawazo ya wanasosholojia ni wazi kwamba unapaswa kuangalia jamii husika, utendaji na dhima ya fasihi katika jamii husika, kwani mihimili hii ndiyo chanzo au historia ya fasihi simulizi ya jamii husika. kutokana na mawazo ya wananadharia hii ni wazi kwamba asili ya fasihi simulizi ya kiafrika ni ndani ya jamii za Kiafrika zenyewe na singinevyo.


Nadharia ya Utaifa. Nadharia hii ilizuka kwenye vugu vugu la kudai Uhuru Barani Afrika. Wanautaifa wanadai kuwa wananadharia wa nadharia ya utandawazi hawakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu lugha za kiafrika, Kwa kiwango kikubwa waliathiriwa na dhana za kikoloni na upendeleo wa kibepari kuwa Afrika ni bara la giza na la washenzi wasiokuwa na aina yoyote ya ustaarabu na walistahili kustaarabishwa na wazungu kupita mlango wa ukoloni.


Nadharia ya Utaifa. Imeasisiwa na S. Adeboye, Babalola, Daniel P. Kunene na J. P Clark. Katika ndharia hii wamejaribu kuondoa dosari ambazo nadharia zilizopita zimeshindwa kuondoa. Kutokana na kwamba wananadharia waliopita mara baada ya kutafiti hawakuwa tayari kuchapisha matokeo yao halisi ya utafiti bali kuyahariri matokeo yao. Na wanaona ni kosa kubwa kufanya utafiti bila kuwahusisha wahusika wa eneo la utafiti.


Hivyo Ili kufahamu vyema historia ya fasihi simulizi ya kiafrika ni lazima kuhusisha wataalamu na wanazuoni wa taifa au jamii hiyo. Kwasababu wataalamu na wanazuoni hao ndio wenye ujuzi wa lugha, utamaduni na historia ya jamii hiyo.


Kiujumla wananadharia ya kitaifa wanaamini kuwa chimbuko la fasihi simulizi ya kiafrika inapatikana ndani na jamii ya kiafrika na ili kuchunguza fasihi ya jamii husika sharti wataalamu na wanazuoni wa jamii hiyo wahusishwe.


Nadharia Hulutishi. Nadharia hii iliasisiwa na wanazuoni wa kiafrika wenye mtazamo kuwa hata wageni wamechangia sana katika kukuza taaluma ya fasihi ya kiafrika. Wanandharia hawa wanaona kuwa fasihi ya kigeni na ya kijadi zimeathiriana na kuingiliana. Miongoni mwa waasisi na wafuasi wa nadharia hii ni pamoja na M.M. Mlokozi, Johnson na Ngugi wa Thiong`o. Hivyo basi historia ya fasihi simulizi ya kiafrika inaweza kujadiliwa kwa kuhusisha au kuchanganya mawazo ya wataalamu wote wa kigeni na wakijadi.


Kwa ujumla nadharia zote tatu zimejaribu kuangalia chimbuko la fasihi simulizi na kutoa muelekeo kuhusu asili ya fasihi simulizi ya kiafrika, Hata hivyo fasihi simulizi ya kiafrika ilikuwepo hata kabla ya ujio wa wageni lakini ilianza kupata athari mara baada ya ujio wa wageni, athari na muingiliano wa fasihi simulizi hauoneshi kuwa fasihi imeanzia sehemu gani kwakuwa fasihi yoyote lazima iathiriwe na iathiri fasihi nyingine. Hivyo basi kila jamii au taifa huwa na fasihi yake na utamaduni wake ambapo maingiliano ya watu na tamaduni zao huweza kuathiriana na hivyo kuathiri pia fasihi ya jamii husika.




MAREJEO.


Materu, M. (1983). “Fasihi simulizi na uandishi wa Kiswahili katika Fasihi,” Makala ya semina za Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili. Dar es Salaam: TUKI.


Mlokozi, M. M. (1996). Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam. TUKI.


Okpewho, I. (1992). The study of Oral Litereture. Bloomington and Indianapolis. Indians: University Press.
















COMMENTS

BLOGGER
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,2861,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Fasihi simulizi na Chimbuko la Riwaya
Fasihi simulizi na Chimbuko la Riwaya
Antagon Blog
http://antagonf.blogspot.com/2014/01/fasihi-simulizi-na-chimbuko-la-riwaya_5279.html
http://antagonf.blogspot.com/
http://antagonf.blogspot.com/
http://antagonf.blogspot.com/2014/01/fasihi-simulizi-na-chimbuko-la-riwaya_5279.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy